top of page

Afya ya Mtoto

Manjano kwa mtoto mchanga (neonatal jaundice)

Manjano kwa mtoto mchanga (neonatal jaundice)

Manjano kwa mtoto mchanga, au njano kwa kichanga, ni ngozi na macho kuwa ya njano kwa sababu ya bilirubini nyingi kwenye damu. Watoto wengi hupata manjano kidogo kuanzia siku ya pili au ya tatu, na huisha yenyewe ndani ya wiki moja au mbili. Manjano yanayoanza ndani ya masaa 24 ya kwanza, yanayofika viganja na nyayo, au mtoto asiyenyonya vizuri, yanahitaji hospitali siku hiyo hiyo.

Mazoezi ya kumlaza mtoto kwa tumbo (tummy time)

Mazoezi ya kumlaza mtoto kwa tumbo (tummy time)

Mazoezi ya kumlaza mtoto kwa tumbo ni kumweka mtoto kifudifudi akiwa macho, mtu mzima akimwangalia, ili aimarishe misuli ya shingo, mabega, mgongo na mikono. Anza siku za mwanzo baada ya kuzaliwa kwa dakika 1 hadi 3, mara kadhaa kwa siku, ukiongeza taratibu hadi angalau dakika 30 kwa siku nzima kufikia miezi 3 hadi 4. Mtoto akilala usingizi, mlaze chali kila mara.

Kubemenda mtoto

Kubemenda Mtoto

Kubemenda ni imani kwamba mtoto anayenyonya hudhoofika mama akishiriki tendo la ndoa mapema baada ya kujifungua, na mwanaume mwingine, au akipata mimba mpya. Hakuna ushahidi kwamba tendo la ndoa lenyewe huharibu maziwa. Mtoto anayekonda, kuharisha au kudumaa ana sababu halisi zinazotibika, kama lishe duni, maambukizi au kuachishwa kunyonya ghafla, na mama anahitaji msaada, si lawama.

Mtoto Kusaga Meno Akiwa Usingizini: Sababu, Madhara na Namna ya Kumsaidia

Mtoto kusaga meno akiwa Usingizini

Kunaweza kuhusishwa na msongo wa mawazo, mabadiliko ya usingizi, ukuaji wa meno au baadhi ya matatizo ya kiafya, na mara nyingi hali hii hupungua kadiri mtoto anavyokua. Msaidie kwa kuweka utaratibu mzuri wa kulala na kupunguza msongo wa mawazo na mpeleke kwa daktari ikiwa hali inaendelea, meno yanasagika, ana maumivu ya taya au kichwa, au anakoroma sana na kupumua kwa shida akiwa usingizini.

Je, vichochea mzio kutoka kwenye maziwa ya ng’ombe vinaweza kupita kwenye maziwa ya mama na kumwathiri mtoto anayenyonya?

Je, vichochea mzio kutoka kwenye maziwa ya ng’ombe vinaweza kupita kwenye maziwa ya mama na kumwathiri mtoto anayenyonya?

Protini za maziwa ya ng’ombe zinaweza kupita kwa kiasi kidogo kwenye maziwa ya mama na kusababisha mzio kwa baadhi ya watoto, ingawa hali hii si ya kawaida na dalili zake zinaweza kufanana na matatizo mengine. Mama anapaswa kuendelea kunyonyesha, kutafuta ushauri wa daktari ikiwa mtoto ana dalili zinazotia shaka na kuepuka maziwa ya ng’ombe kwa muda tu ikiwa inashauriwa baada ya tathmini ya kitaalamu.

Mtoto kunyonya Vidole

Mtoto kunyonya Vidole

Kunyonya vidole ni tabia ya kawaida kwa watoto wadogo; humsaidia mtoto kujituliza, na wengi huiacha wenyewe kati ya miaka 2 na 4. Kunyonya kwa nguvu na kwa muda mrefu, hasa meno ya kudumu yanapoanza kuota, kunaweza kusogeza meno na kubadilisha umbo la taya. Msaidie kwa upole, pongezi na shughuli mbadala, bila adhabu, na mwone daktari wa meno ikiwa tabia inaendelea baada ya miaka 3.

bottom of page