Mwandishi:
Mhariri:
Imeandikwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
30 Oktoba 2026, 15:05:58
Namna ya Kuweka App ya ULY CLINIC kwenye simu

Jinsi ya kupakua na kusakinisha App ya ULY CLINIC
Hatua ya 1:
Bofya "Pakua App ya ULY CLINIC". Faili litaanza kupakuliwa kwenye simu yako.
Kivinjari (mfano Chrome) kikikuonyesha ujumbe kama "Faili hili linaweza kudhuru kifaa chako", bofya "Pakua hata hivyo" (Download anyway). Ujumbe huu hutokea kwa kila app isiyopakuliwa kutoka Play Store. App yetu ni salama.
Hatua ya 2:
Fungua faili Upakuaji ukiisha, bofya "Fungua" (Open). Au fungua sehemu ya Vipakuliwa (Downloads) kwenye simu yako na ubofye faili la ULY CLINIC.
Hatua ya 3:
Ruhusu "Sakinisha programu zisizojulikana" Mara ya kwanza, simu inaweza kukuambia: "Kwa usalama wako, simu yako hairuhusiwi kusakinisha programu zisizojulikana kutoka chanzo hiki" (Install unknown apps). Usiogope, fanya hivi:
Bofya "Mipangilio" (Settings).
Washa kitufe cha "Ruhusu kutoka chanzo hiki" (Allow from this source).
Bonyeza kitufe cha kurudi nyuma (◁) kwenye simu yako.
Ruhusa hii inahitajika mara moja tu.
Hatua ya 4:
Sakinisha Bofya "Sakinisha" (Install) na usubiri sekunde chache.
Ukiona ujumbe wa Google Play Protect kama "App hii haijulikani", bofya "Maelezo zaidi" (More details), kisha "Sakinisha hata hivyo" (Install anyway).
Hatua ya 5:
Fungua app Bofya "Fungua" (Open). App ya ULY CLINIC itaonekana pia kwenye skrini ya simu yako.
Kama tayari una App ya ULY CLINIC
Usiifute app ya zamani. Pakua toleo jipya na usakinishe juu yake. Taarifa zako zitabaki salama.
Ukiona aikoni mbili za ULY CLINIC baada ya kusakinisha, futa ile ya zamani tu.
Unahitaji msaada?
Wasiliana nasi kwa namba za simu zilizo chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa
30 Oktoba 2026, 15:14:23


