top of page

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

Namna ya kutunza au kujitunza kwa mtu mwenye tatizo la ualbino

Tatizo la u albino huambatana na madhaifu kwenye ngozi na macho

Mtu mwenye u albino anaweza kupata matibabu ya mazingira kwa ajiri ya kupunguza au kuepuka madhara yanayoweza kutokea. kama yaliyoorodheshwa hapa chini.

Kujikinga na mwanga wa jua

Wagonjwa wenye tatizo la ualbino wa macho,  macho yao yanahitaji kukingwana mwanga mkali wa jua katika maisha yao yote. Wazazi na wa athirika wa tatizo hili wanahitaji kufundishwa namna ya kujikinga au kukabiliana na mwanga wa jua kwa njia zifuatazo

  1. Kuvaa miwani

  2. Kupenda Kukaa kivulini kuepuka mionzi ya mwanga wa jua

  3. Kuvaa nguo za kujikinga na mionzi ya jua, kama vile kofia na nguo za mikono mirefu, nguo maalumu zenye uwezo wa  kupunguza mionzi ya mwanga wa jua, shati yenye kola

  4. Angalau kuwa na masaa mawili kila baada ya muda Fulani kukaa mbali na mwanga wa jua wa moja kwa moja

  5. Kuzuia kutumia dawa zinazoweza ongeza hisia ya ngozi kwenye mionzi ya jua

Kumwona daktari

Watu wenye ualbino wanatakiwa kumwona daktari kila baada ya miezi 6 hadi 12 kufanyiwa vipimo na uchunguzi wa ngozi. Uchunguzi wa ngozi husaidia kutambua saratani ya ngozi mapema zaidi, mwathirika atatakiwa kufanya hivi kwa sababu huwa kwenye hatari ya kupata saratani ya ngozi. Uchunguzi huu ni kwa ajili ya watoto wadogo chini ya miaka 13.

Watu wazima wanatakiwa kuhudhuria clinic kila baada ya miaka mitatu hadi sita kufanyiwa uchugnuzi huu.

ULY Clinic inakukumbusha kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yale yanayohusu afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kupiga namba za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

Rejea za mada

Imeboreshwa 24.03.2020

bottom of page