Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
​
Alopesia
​
Alopesia ni tatizo la kunyonyoka kwa nywele za kichwani au maeneo mengine ya mwili, tatizo hili husababisha upara kichwani na maeneo mengine ambayo yalikuwa na nywele na sasa hayana. Alopesia huweza kuwa ya muda au ya kudumu. Alopesia ya muda inaweza kusababishwa na dawa au madhara ya tiba kama vile tiba ya mionzi, dawa jamii ya saitotoksiki, dawa za kuyeyusha damu, dawa jamii ya retinoidi, dawa jamii ya beta bloka, na dawa za vidonge vya uzazi wa mpango kwa magonjwa ni kama vile tatizo la fangasi kichwani(tinea kapitis) au mashiringi kichwani.
​
Alopesia inaweza kusababishwa na
Alopesia ya mabadiliko ya kukua- nywele huanza kuwa nyepesi jinsi umri unavyoongezeka, haya ni mabadiliko ya kawaida kutokea kwa jinsi mtu anavyoongezeka umri.
Alopesia ya androjeni- huathiri watu wa jinsia zote, hutokea mapema sana kwa wanaume na wanawake hata wakati wa ujana unapoanza kwenye miaka ya ishirini. Upara husababisha kupotea kwa nywele kuanzia mbele ya kichwa kurudi nyuma.
​
Alopesia areata- kupoteza nywele kwa Watoto wadogo na wale wanaoelekea kuwa watu wazima, kisababishi huwa hakifahamiki, huanza ghafla na huweza kuishia kupoteza nywele zote kabisa za kichwani. Asilimia 90 ya wagonjwa huota nywele tena baada ya miaka kadhaa
Alopesia univezaliz,- kupoteza nywele zamwili bila sababu ya kujulikana, kuna uwezekano mdogo sana wa nywele kuota tena, haswa kwa Watoto wadogo
Magonjwa ya mwili kujishambulia wenyewe- mfano ugonjwa wa Lupasi erizimatosasi
​
Soma zaidi kuhusu dalili na matibabu ya alopesia kwa kubonyeza hapa
​
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii
​
​
Imeboreshwa 10.03.2020
Rejea
-
Ulyclinic