top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Sima A, CO, Dkt. Benjamin L, MD

27 Oktoba 2020 08:15:22

Mifupa ya kifua (Mbavu)
Mifupa ya kifua (Mbavu)
Mifupa ya kifua (Mbavu)

Mifupa ya kifua (Mbavu)

Kuna jumla ya mifupa 12 ambayo inatengeneza kifua, Mifupa hii imeungana na uti wa mgongo kwa nyuma na mbele imeunganishwa na kifua kupitia cartilage


Makundi ya mbavu


Mifupa ya Mbavu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni:


 • Mbavu halisi

 • Mbavu isiyo halisi


Mbavu halisi:

Ni mifupa ambayo inayo kichwa, shingo na mwili


Kichwa: Ni sehemu ambayo inaungana na uti wa mgongo inayo umbo la mduara lenye vifundo fundo


Shingo: Ni sehemu ambayo haina mnyanyuko, huunganisha kichwa na mwili wa mbavu


Mwili wa mbavu: Ni sehemu ambayo ipo tambarale na yenye mfumo wa neva na mishipa ya damu. Hutumika katika kulinda neva hizo pamoja na mishipa ya damu


Mbavu isiyo halisi

Huhusisha mbavu namba 1,2,10,11 na 12 ni mifupa ambayo huelezeka kama mifupa ambayo siyo halisi kwa kukosa sifa mojawapo ya kuwa na kichwa, shingo au mwili


Mbavu ya kwanza:

Mbavu hii huwa fupi na pana kuliko mbavu zingine na pia hii imepitiwa na mshipa mkubwa wa damu wa subclavian


Mbavu ya 2:

Mbavu hii ni nyembamba na ndefu kuliko mbavu ya 1, mbavu hii hushikiria misuli ya serratus


Mbavu ya 10:

Mbavu hii ina facet moja ambayo huifanya kuungana na uti wa mgongo


Mbavu ya 11 na 12:

Mbavu hii haina shingo na inayo facet moja tu ambayo huifanya kuungana na mifupa ya uti wa mgongo


Mifupa yote 12 ya mbavu inaungana kwa nyuma na mifupa ya uti wa mgongo na kutengeneza jointi ambazo ni:


 • Jointi ya Kostotransvesi: Ni jointi kati ya mbavu na uti wa mgongo

 • Jointi ya Kostovetebro: Ni jointi kati ya kichwa cha mbavu kwa juu na sehemu ya chini ya mifupa uti wa mgongo


Kwa mbele mifupa imeungana na sehemu zifuatazo ambazo ni :


 • Mbavu ya kwanza na ya pili: Mbavu hizi zimeungana kwa mbele na mfupa sternum

 • Mbavu ya 8 na 10: Mbavu hizi zimeungana na cartilage kwa sehemu ya juu

 • Mbavu ya 11 na 12: Mbavu hizi zimeungana Pamoja sehemu ya mbele na huwa chini ya kifua yaani sehemu ya tumbo

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.

Imeboreshwa,

25 Septemba 2021 10:49:58

Rejea za makala hii,

 1. TeachMeAnatomy.RibsAnatomy.https://teachmeanatomy.info/thorax/bones/ribcage/. Imechukuliwa 6/10/2020

 2. Kenhub.RibsAnatomy.https://www.kenhub.com/en/library/anatomy/the-ribs. Imechukuliwa 6/10/2020

 3. Britanica.RibsAnatomy.https://www.britannica.com/science/rib-cage. Imechukuliwa 6/10/2020

 4. RegisteredNurse.RibsAnatomy.https://www.registerednursern.com/ribs-anatomy/. Imechukuliwa 6/10/2020

bottom of page