top of page
© Hairuhusiwi kukopi bila kibali cha ULYCLINIC

Anatomia

Anatomia katika makala hii imetumika kumaanisha maumbile mbalimbali ya viungo vya binadamu. Bonyeza soma zaidi ili kusoma maumbile ya kiungo ulichochagua

Miili ya kavenasi

Miili ya kavenasi

Miili ya kavenasi ni miundo miwili mirefu ya tishu maalumu za kusimamisha uume inayopatikana ndani ya shina la uume, upande wa kulia na kushoto, na ambayo hujaa damu wakati wa msisimko wa kingono na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kusimama na kuwa mgumu kwa uume. Kwa pamoja, miili hii miwili ndiyo sehemu kuu ya tishu za kusimamisha uume.

Misuli ya bulbospongiosi

Misuli ya bulbospongiosi

Ni jozi ya misuli ya sakafu ya nyonga inayopatikana katika sehemu ya chini ya nyonga, karibu na mzizi wa uume kwa mwanaume na karibu na sehemu ya chini ya uke kwa mwanamke. Misuli hii ni sehemu ya misuli ya eneo la kati ya mapaja ikifahamika kama msamba au periniamu na hufanya kazi muhimu katika mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi.

Anatomia ya Kisimi

Anatomia ya Kisimi

Kisimi ni kiungo cha mwili wa mwanamke ambacho kina jukumu muhimu katika msisimko wa kimapenzi. Ni sehemu yenye neva nyingi zaidi mwilini, na hivyo ni nyeti sana kwa mguso. Ingawa sehemu ya nje ya kisimi inaweza kuonekana kwa macho, sehemu kubwa ya muundo wake ipo ndani ya mwili.

Anatomia ya Ulimi

Anatomia ya Ulimi

Ulimi ni kiungo cha mwili kinachohusika katika kuhisi ladha ya chakula na pia kufanya mtu aweze kuumba maneno na kuyatamka, kiungo hiki huanza kuumbwa siku ya 23 kwa kijusi aliye tumboni mwa mama.

Mifupa ya Mkono

Mifupa ya Mkono

Mkono umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni sehemu ya juu ya mkono ambayo ipo katikati ya bega na kiwiko, sehemu ya kati ya mkono ambayo ipo katikati ya kiwiko na jointi za viganjani na sehemu ya mwisho ni kiganja cha mkono. Tazama picha kwa kuelewa zaidi

bottom of page