top of page

Imeandikwa na mfamasia wa ULY CLINIC

 

Clomiphene

Ni dawa ambayo ipo kwenye kundi la selestive Estrogen receptor modulator, dawa zingine zilizo kwenye kundi hili ni pamoja na bazedoxifene/conjugated estrogens, Clomid, clomiphene, Duavee, Evista, ospemifene, Osphena, raloxifene, Serophene na tamoxifen.

Dawa hii hutumika kuongeza uzalishaji wa mayai kwa wagonjwa wenye tatizo la polisistiki ovarian sindromu na wanwake wenye matatizo ya ugumba

 

Hupatikana kama kidonge cha miligramu 50 na 100

Baadhi ya maudhi madogo ya  dawa kwa baadhi ya watu ni pamoja na;

  • Kukua kwa ovari

  • Kutokwa na jasho

  • Mvurugiko wa hali ya tumbo

  • Kuona malengelenge

  • Kichefuchefu na kutapia

  • Mvurugiko wa hali ya titi

 

Maudhi mengine ambayo yalijulikana baada ya dawa kuingia sokoni ni;

 

Kwenye mfumo moyo na mishipa ya damu: arizmia, shinikizo la juu la damu, embolizim ya palmonari, mapigo ya moyo kwenda haraka au taratibu, thromboflebaitis, kuishiwa pumzi.

Ngozi: chunusi, mzio, erizima, erizima matifomi, erizima nodosa, haipatrikosis, miwasho na utikaria.

Mfumo wa mkojo na uzazi. Endometriosis, isti ya ovari, kukua kwa ovari, hemoreji ya ovari, ujauzito kwenye mirija ya uzazi, kupungua kwa upana wa endometria.

Imeboreshwa 5.03.2020

Rejea

BNF 78 edition 2019

bottom of page