top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

 

Dawa za kutibu PID

 

PID ni maambukizi ya bakteria katika mfumo wa juu wa uzazi, hii huhusisha mfuko wa kizazi, mirija ya uzazi na sehemu za mayai na zile zinazozunguka nje ya mfuko wa kizazi kwa jina tiba la peritoneum. PID hutokea endapo matibabu ya magonjwa ya zinaa hayajafanyika vema au mtu hajatibiwa kabisa baada ya kupata magonjwa ya zinaa. Kulingana na miongozo ya nchi mbalimbali.

 

Soma zaidi kuhusu PID na dalili zake ndani ya tovuti ya ULY CLINIC kwa kubonyeza hapa.

 

Dawa zilizoorodheshwa hapa chini huwa hazitumiki zote kwa pamoja kwenye matibabu ya PID. Matibabu ya PID yanahitaji kutumia dawa mbili au tatu kati ya zilizoorodheshwa ili kutibu ipasavyo tatizo hili. Kwa wagonjwa wa PID wenye aleji/mzio na dawa aina fulani kati ya zilizooroheshwa hapo chini wanapaswa wasitumie dawa hizo. Hata hivyo kuna baadhi ya watu maambukizi yao ni sugu hivyo huhitaji kufanayiwa uchunguzi zaidi kabla ya kuanza dawa.

 

Dawa zinazotumika kwenye matibabu ya PID  zinaweza kuwa kwenye fomu ya dawa za kuchoma au dawa za kunywa ambazo ni;

​

 

Kumbuka:

​

  • Dawa zilizoorodheshwa hapo juu hutumika kwa kuandikiwa na daktari tu

  • Matumizi ya dawa pasipo kuandikiwa na daktari hupelekea usugu wa bakteria dhidi ya dawa hiyo

  • Vimelea vikitengeneza usugu kwenye dawa, dawa hiyo haitafaa kamwe kwenye mwili wako kwa matibabu ya PID

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale baada ya kusoma makala hii

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na Tiba kwa kubonyeza ‘Pata tiba’ au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

 

Rejea za mada hii

 

  1. Pelvic Inflammatory Disease (PID). https://www.cdc.gov/std/tg2015/pid.htm. Imeandikwa 8.12.2020. Imechukuliwa 8.12.2020

  2. Pelvic Inflammatory Disease (PID) Treatment and Care. https://www.cdc.gov/std/pid/treatment.htm. Imechukuliwa 8.12.2020

  3. Pelvic Inflammatory Diseasehttps://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK499959/. Imechukuliwa 8.12.2020

  4. What's the Treatment for Pelvic Inflammatory Disease?. https://www.webmd.com/women/guide/treatment-pelvic-inflammatory-disease. Imechukuliwa 8.12.2020

bottom of page