Imeandikwa na daktari wa ULY clinic
Vidole rungu
Vidole rungu hutokana na kukuwa kwa miishio ya vidole. Visababishi vyake havinauhakika lakini inasemekana huweza kusababishwa na hypoksia na homoni ya eithropoietin kwenye damu.
Vidole kuwa rungu huweza kurithiwa lakini mara nyingi huwa ni tatizo la kupata baada ya kuzaliwa.
Visababishi kutokana na mifumo ya mwili huwa pamoja na;
Mfumo wa upumuaji
-
Saratani ya mapafu
-
Bronkolaitiz
-
Alveolaitiz ya faibrozing
-
Asbestosis
-
UKIMWI, Maambukizi ya fangasi na maicoplasma
-
Mesothelioma
Mfumo wa Kadiovasikula
-
Endokadaitis
-
Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo
Mfumo wa Gastointestino
-
Colaitiz ya vidonda
-
Ugonjwa wa Crohn
-
Ugonjwa wa seliaki
-
Ugonjwa wa Ini
Magonjwa ya metaboliki
-
Akromegali
-
Thairotoksikosis
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba