Maambukizi kwenye koromeo-Pharyngitis
Imeandikwa na madaktari wa ULY-CLinic
Utangulizi
Maana na Kisababishi
Maambukizi kwenye koromeo kwa watoto husababishwa kwa asilimia kubwa na virusi kama adenovirus, coronavirus, enterovirus, rhinovirus RSV, EBV, HSV, metapneumovirus pamoja na bakteria kundi A B hemolytic streptococcus. Bakteria wengine pia wanaweza kusababisha maambukizi katika koromeo.
Ukubwa wa tatizo
Maambukizi ya virusi katika mfumo wa juu wa hewa huambukiziwa kwa njia ya kukaa karibu na mtu anayeumwa haswa katika majira ya baridi na kucipua. Maambukizi a streptococcal hayatokei kwa watoto sana kabla ya kufikisha umri wa miaka 2 hadi 3, hutokea sana kipindi wakianza kwenda shule na hupotea kwenye ujana na utu uzima. Maambukizi hutokea majira ya kuchipua na baridi na husambaa kati ya wanafunzi marafiki au ndugu wanaoishi pamoja.
​
​
Dalili
Ugonjwa hutokea haraka baada ya maambukizi na huambatana na dalili zifuatazo kama imesababishwa na bakteria;
-
koo kukauka,
-
kikohozi
-
homa.
-
Kichwa kuuma
-
Dalili za tumbo kama maumivu ya tumbo na kutapika hutokea mara kwa mara
Uchunguzi wa koo huonesha dalili za kuwa jeundu sana, tezi za tonsili huonekana zimekua na zinaweza kuwa zimefunikwa na utando wanjano wenye damu kidogo
Dalili za maambukizi ya virusi katika koromeo ni;
-
Kuchuruzika kwa mafua
-
Kikohozi
-
Kuharisha
-
Macho pia huuma
-
Sauti kubadilika(kama ya punda)
Kila kirusi aliyetajwa anaweza kuwa na dalili yake ya kipekee ila kwa ujumla dalili hizo hutokea endapo mtu amepata maambukizi ya virusi katika koo.
​
Vipimo na uchunguzi
Malengo ya uchunguzi ni kujua sana kinachosababisha maambukizi ya koromeo ni nini haswa. Dalili za maambukizi ya koromea ya bakteria na virusi huwa na mwingiliano hivyo ni vigumu kujua ni nini kilichosababisha. Hata hivyo daktari atatia mkazo sana kuwa maambukizi yamesababishwa na bakteria aina ya streptococcal kwa mtoto ili kutibu na kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na bakteria hao katika moyo.
Kipimo cha kuotesha bakteria
Kipimo hiki hufanyika kwa kuchukua majimaji kutoka katika koo na kasha kuotesha maabala, bakteria anayetambuliwa hutibiwa kulingana na dawa iliyo na nguvu kupambana na bakteria huyo. Lakini kipimo hichi pia kinaweza kisitambue bakteria hawa au mtoto anaweza kuwa mbebaji wa bakteria lakini sio wenyewe walio sababisha maambukizi katika koromeo.
Kipimo cha antigeni
Kipimo hiki ni kizuri kwani hutambua antigeni ya bakteria, huwa cha haraka na kinasaidia kuondoa utata wa kipimo cha kuotesha bakteria kama kilivyoelezewa hapo kabla.
Vipimo vingine
Kipimo cha kuangaliwa sifa za chembe za damu huwezakusaidia kutambua aina zingine za maambukizi endapo maambukizi yamesababishwa na bakteria au kirusi.
Kwa ujumla kwenye taasisi ambazo hazijiwezi kivifaa na hazifanyi huzuma za kupima, ni bora kuwa na shuku kubwa kwamba maambukizi ya koromeo yamesababishwa na bakteria aina ya streptococcal na kuanzisha matibabu dhidi ya bakteria hoa kwa watoto ili kuzuia madhara yanayowezakuwa hatari kwa mtoto.
Matibabu
Kama matibabu yasipofanyika, maambukizi mengi huisha ndani ya siku chache, lakini kuanza mapema kwa dawa za kupambana na bakteria huharakisha unafuu ndani ya masaa 12 hadi 24. Madhumuni ya awali ya matibabu ni kuzuia madhara yanayoweza kusababisha homa ya rheumatizimu ya moyo, ambayo huweza kuzuia endapo maambukizi yatatibiwa ndani ya siku 9 ya maambukizi ya koromeo. Matibabu hufanyika papo kwa hapo baada ya kipimo cha antigen bila kusubiri majibu ya kuotesha. Endapo taasisi haifanyi vipimo hivi basi matibabu huanza mara moja mara ugonjwa unapotambuliwa.
Madhara na kinga
​
Maambukizi ya virusi kwenye koromeo huweza kusababisha maambukizi ya bakteria katika mfumo wa kati wa masikio, jipu kwenye koromea na homa ya rheumatizim ya moyo hutokana na maambukizi ya bakteria katika koo.
​
Kinga
​
Kupata chanjo kwa watoto dhidi ya bakteria hawa. Dawa kinga pia dhidi ya maambukizi ya kujirudia rudia kwa kutumia penicillin, lakini hutumika tu kuzuia maambukizi ya mda mfupi ya rheumatizimu ya moyo kama yanajirudia rudia.
Imechapishwa 3/3/2015