top of page

Matibabu ya kisukari aina ya 2

 

Imeandikwa na Dr. Mangwella sospeter(MD)

​

Shirika la dawa na chakula duniani FDA limependekeza matumizi ya dawa za vidonge aina mbili tofauti mara moja kwa siku kukabiliana na sukari kwa mgonjwa wa kisukari aina ya 2. Mchanganyo wa dawa mbili zilizopendekezwa ni dawa kundi la sodium glucose cotransporter na mertformin. Vidonge vinatakiwa vitumike pamoja na mazoezi kwa mtu mwenye kisukari na dawa zinatakiwa zitumiwe asubuhi baada ya kula chakula.

 

Lengo la matibabu ya kupambana na kupanda kwa sukari ni;

  • Kupunguza hatari ya uharibifu katika mishipa midogo ya damu inayoweza kuathiri utendaji kazi wa Macho na figo

  • Kupunguza hatari ya uhalibifu wa mishipa mikubwa ya damu inayoweza kusababisha magonjwa ya mishipa ya moyo,ubongo, na maeneo ya miguuni

  • Kupunguza madhara ya kimfumo wa fahamu na utendaji kazi wa chembe hai

​

​

Kiwango cha sukari

Kutumia dawa bila kutazama matokeo ya dawa kwenye kiwango cha sukari katika damu huwa haisaidii. Ni vema kupima kiwango cha sukari kwa sababu

  • Husaidia kutambua kiwango cha sukari kwenye mda huo utakaopima

  • Kutambua kama una kiwango cha juu au cha chini kwenye mda husika

  • Kuonyesha kwa namna gani mazoezi dawa au kubadili mfumo wa maisha yako umesaidia kukabili tatizo la sukari kwenye damu

  • Kumsaidia daktari au mtaalamu wako wa kisukari kukupa ushauri na kubadili au kuongeza dozi ya dawa ili kuimarisha au kufikia kiwango cha kawaida cha sukari.

​

1.Mara ngapi upime kiwango cha sukari?

​

Ni mara ngapi upime kiwango cha sukari katika damu hutegemea mpango wa matibabu yako. Wewe na mtaalamu wa kisukari mtashauriana mara ngapi upime kiwango chako cha sukari. Lakini hapa chini ni utaratibu unaweza kuufanya kwa matokeo mazuri zaidi, kumbuka kuandika matokeo ya vipimo katika daftari au kitabu chako cha kipimo cha sukari, usisahau kuweka tarehe na mda uliopima.

  1. Kabla ya mlo wowote(wa asubuh, mchana na usiku,)

  2. Kabla ya kulala

  3. Masaa 2 au 3 baada ya kula

  4. Sa nane au tisa usiku(fanya hili mara moja kwa wiki)

  5. Ukiwa unaumwa

  6. Kabla ya kuendesha gari

  7. Unapoanza kufanya mazoezi

  8. Kama ukiamka na kiwango kidogo au cha juu cha sukari

  9. Kama ukibadili dozi ya insulin, dawa au mazoezi

  10. Ukipata ujauzito au ukiwa na mpango wa kupata ujauzito

  11. Kama ukiwa na shida ya kutambua dalili za kushuka kwa sukari katika damu

Kupima sukari mara kwa nyakati zilizozungumziwa hapo kunasaidia sana kudhibiti sukari kwa sababu ni rahisi kujua sukari inapanda au inashuka wakati gani na mtashauriana na daktari wako nini cha kufanya kulingana na matokeo ya vipimo vyako.

​

2.Unapimaje kiwango cha sukari?

​

Kipimo cha glucometa kinachopatikana kwa majina tofauti kama (glucoplus, accutrend, glucotrend n.k) hutumika kupima kiwango cha sukatri katika damu ukiwa nyumbani. Ongea na daktari wako au mfamasia ili akuchagulie kilicho sahihi kwako na ambacho upatikanaji wa strips za kupimia ni rahisi katika eneo lako. Ukipata mashine yako basi hakikisha unapata maelekezo muhimu kabla ya kuanza kuitumia.

Mwulize mtaalamu wa afya kuhusu sehemu gani na mahali gani mwilini mwako pa kutoa damu ya kupima, kiwango cha damu cha kutoa, jinsi ya ku safisha mashine yako, jinsi ya kutazama kama mashine yako inafanya kazi na jinsi ya kutumia code ya mashine yako.

​

​

3.Jinsi ya kufikia malengo ya kiwango cha sukari kinachohitajika(rejea)

Kama una kisukari, unatakiwa kuhakikisha kiwango chako cha sukari kipo karibu na kiwango rejea kwa jinsi inavyowezekana. Kufanya hivi itasaidia kupunguza madhara ya kisukari mwilini. Kuwa na tabia ya Kula kiafya kila siku, kutumia dawa kama ni lazima, itakusaidia kuweka kiwango cha sukari yako katika kiwango rejea.

  • Kiwango rejea cha sukari hutofautiana, hutegeea umri , hali ya kiafya na vihatarishi vingine.

  • Kiwango rejea kwa wamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 12 huwa tofauti. Mwulize mtaalamu wako wa afya akuambie kiwango cha kawaida unachotakiwa kuwa nacho

​

Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote

​

Pata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshwa 12.03.2020

​

Rejea​

Matibabu yakisukari aina ya 2
Kiwango cha sukari
Mara ngapi kupima sukari?
Unapimaje kiwango cha sukari?
Kufikia malengo ya kiwango cha sukari
bottom of page