Vipimo na utambuzi wa kisukari
Imeandikwa na daktari wa ULY clinic
Vipimo vinavyofanyika
Je vipimo gani hufanywa ukiwa hospitali?
-
Kipimo cha sukari kabla hujala kitu chochote asubuhi toka ulipokula usiku wa kuamkia siku hiyo (fasting blood glucose-FBG)
-
Kipimo hiki husomwa kwa vizio vya aina mbili ( mg/dl au mmol/L ), utasemekana sukali yako ipo juu endapo kipimo kikizidi miligramu 126 kwa kila desilita 1 ya damu (yaani 126mg/dl) au milimole 7 kwa kila lita moja ya damu (yaani 7mmol/L)
-
-
Sukari kuwa 200mg/dl(11.1mmol/L) au zaidi baada ya masaa mawili ya kupewa sukari yenye gramu 75- kipimo hiki huitwa oral glucose torelance test (OGTT)
-
Sukari kuwa zaidi ya 200mg/dl(11.1mmol/L) au zaidi unapopimwa ukiwa ushakula au kwa jina jingine “Rondum blood glucose”-RBG
-
Kipimo kingine ni cha kiwango cha sukari kwenye chembe za damu za hemoglobin A1c (HBA1c) ambapo ikiwa asilimia 6.5 au zaidi mtu anaitwa anakisukari
Mtu mwenye sifa zifuatazo anatakiwa kuwa anapima kisukari hata kama hana kisukari
-
Shinikizo la damu kuwa juu zaidi ya 135/80mmHg
-
Uzito kupita kiasi au ana vihatarishi kama vya kupata kisukari kama(kuwa na ndugu wa baba/mama mmoja mwenye kisukari, shinikizo la damu zaidi ya 140/90 na kiwango cha lehamu nzuri kwenye damu chini ya 35mg/dl au kiwango cha triglceride kwenye damu zaidi ya 250mg/dl)
-
Kuwa na miaka zaidi ya 45 hata kama hauna sifa za hapo juu
Matibabu ya kisukari
Matibabu ya kisukari ni yapi?
Matibabu ya kisukari hutegemea aina ya kisukari ulichonacho endapo ni aina ya 1 au 2
Matibabu ya kisukari aina ya 1
Matibabu ya kisukari aina ya kwanza huwa ni yale ya kutumia sindano yenye homoni ya insulin, insulin hii hutolewa kulingana na uzito wa mtu na dozi yake ya siku huwa kati ya 0.5- 1 IU kwa kila kilo ya uzito na hutumiwa mchanganyiko wa insulin aina mbili, aina ya kwanza ni lente naya pili ni soluble
Mfano mtu mwenye kilo 60 akitumia dozi ya 0.5 IU/Kg manake dozi yake ya siku nzima itakuwa 30IU yaani (0.5 IU/Kg × 60kg = 30 IU)
Kwa jinsi gani unapata dozi ya asubuhi na jioni na utatumia lente kiasi gani na soluble kiasi gani?
Mahesabu huwa ya namna hii, mara baada ya kupata dozi ya siku nzima kama tulivyopata 30 kwa mtu mwenye kilo sitini endapo atatumia 0.5 IU/Kg basi mbili ya tatu ya dozi (×30 IU =20 IU) hutumika asubuhi na moja ya tatu iliyobaki hutumika jioni ( ×30=10)
Tumepata 20 IU asubuhi na 10 IU jioni basi tuangalie asubuhi unatakiwa kutumia lente kiasi gani na soluble kiasi gani?
Mahesabu ni yale yale ya dozi nzima ya asubuhi huwa lente na ya dozi ya asubuhi huwa soluble.
Dozi ya asubuhi
Sasa tuchukulie kwa dozi yetu ya 20IU ya asubuhi
Lente itakuwa kiasi gani? ( ×20 IU= 13 IU)
Soluble itakuwa (×20 IU= 7 IU) au 20-13=7 IU
Dozi ya jioni nayo hupatikana
ya dozi nzima ya jioni huwa lente na ya dozi nzima ya jioni kuwa soluble.
Kwa dozi yetu ya 10IU kama tulivyopata awali
Lente = ( ×10 IU=6.66 IU au 7 IU)
Soluble= ( × 10 IU= 3.33 IU au 3 IU)
Vitu vya kukumbuka
-
Tumeanza kutumia kiwango cha 0.5 IU kwa kila kilo yako yauzito kama dozi ya siku nzima na sio 0.7 au 0.9 au 1 IU kwa kilo kwa sababu zifuatazo;
-
Ukitumia dozi kubwa ya insulin kwa siku unaweza kusababisha kiwango cha sukari kushuka sana, hali hii inaweza kupelekea kuzimia au kufa endapo matibabu ya haraka hayajafanyika.
-
Ili kama dozi ya chini isiposhusha sukari kwa kiwango kinachotarajiwa au ulichoshauriwa na daktari wako, dozi ipandishwe kwenda zaidi ya 0.5 kwa kila kilo ya uzito wako
-
Mwombe ushauri mtaalamu wa kisukari au daktari wako ili akukokotolee dozi sahihi kulingana na uzito wako endapo hujaelewa mahesabu haya. Pia daktari wako atakushauri ni wakati gani wa kuongeza/ kupunguza dozi ya insulin ili iendane na mahitaji ya mwili wakati huo ikiwa inafanya kazi vema kurekebisha kiwango cha sukari kuwa kwenye hali ya kawaida.
Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote
Imeboreshwa 12.03.2020