top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

ULY Clinic inakushauri kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Maumivu ya hedhi

Maumivu ya hedhi

Maumivu yoyote yale ya hedhi huamshwa na kemikali zinazoitwa prostaglandin na leukotriene katika mfumo wa uzazi ambazo ni kawaida kuzalishwa wakati wa yai kutengenezwa na kutoka kwenye ovari.

Muwasho wa ngozi kutokana na VVU

Muwasho wa ngozi kutokana na VVU

Harara kwenye ngozi inaweza kutokea kwa mtu yeyote yule, hata hivyo harara inayoambatana na muwasho au vipele mara nyingi huwa dalili ya kwanza ya VVU kwa watu walio wengi.

Kupiga miayo mingi

Kupiga miayo mingi

Kupiga mwayo ni kitendo kisicho cha hiari cha kufungua kinywa na kuvuta pumzi kwa kina ili kujaza hewa safi kwenye mapafu. Fanya mazoezi, lala muda wa kutosha na poza mwili kwa upepo au kinywaji cha baridi ili kupunguza miayo mingi.

Dalili za utapiamlo

Dalili za utapiamlo

Utapiamlo ni hali inayotokana na utumiaji wa lishe yenye virutubisho ambavyo havitoshi au lishe iliyozidi, inayopelekea athari kwa afya ya mtoto.

Jipu njia ya haja kubwa

Jipu njia ya haja kubwa

Jipu kwenye njia njia ya haja kubwa ni mkusanyiko wa usaha sehemu ya kupitishia haja kubwa ama ndani ya kifuko kinachotunza kinyesi kabla hakijatoka au maeneo karibu na njia ya haja kubwa.

bottom of page