top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

Dkt. Peter A, MD

21 Novemba 2021, 08:44:45

Muwasho wa ngozi kutokana na VVU
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Muwasho wa ngozi kutokana na VVU

Watu walioambukizwa VVU hupata harara kwenye ngozi muda fulani katika maisha. Harara kwenye ngozi pia inaweza kuwa miongoni mwa dalili za awali za maambukizi ya VVU kwa watu walio wengi au dalili za hatua za mwisho za UKIMWI.


Harara kutokana na maambukizi ya VVU


Harara ya VVU inaweza kusababaishwa na sababu mbalimbali ikiwa pamoja na mwitikio wa kinga ya mwili kwenye kirusi cha UKIMWI, dawa za kufubaza makali ya VVU au magonjwa nyemelezi.


Baadhi ya waathirika wa VVU hupata harara kali zinazohitaji matibabu ya haraka la sivyo maisha ya mwathirika huwa hatarini.


Harara ya mwitikio mkali kwenye maambukizi ya VVU


Maambukizi ya VVU husababisha harara zilizoinuka kiasi juu ya usawa wa ngozi na hutokea sana kwenye kiwiliwili, usoni na wakati mwingine kwenye miguuni na mikononi. Kwa watu wenye rangi nyeupe, harara zinazotokea huwa na rangi nyekundu na watu weusi huwa na rangi kama zambarau.


Kwanini harara hutokea mtu anapopata maambukizi ya VVU?

Harara kwa mtu aliyepata maambukizi ya VVU hutokea kutokana na mwitikio wa kinga ya mwili kwenye virusi. Mwitikio huu huamsha kemikali za mzio zinazoleta harara kwenye ngozi.


Dalili zingine zinaweza kuambatana na harara ambazo mara nyingi hudumu muda wa wiki mbili ni;


  • Homa

  • Uchovu

  • Kuvimba mitoki

  • Vidonda kooni

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya misuli

  • Kuharisha


Wakati wa kuonana na daktari?


Kwa sababu dalili za VVU hufanana na dalili za mafua ya virusi au magonjwa mengine ambazo hupotea wiki chache tu, inaweza kuwa vigumu kugundua kwamba umepata maambukizi ya VVU au la. Hata hivyo kama umekuwa kwenye kihatarishi cha maambukizi na una mashaka ya kuwa umepata VVU, unapaswa kufika kituo cha afya mara moja kwa ushauri na vipimo.


Harara kwenye ngozi kutokana na magonjwa mengine kwa wagonjwa wa UKIMWI


Kama mtu asipopata matibabu au asipozingatia matibabu ya VVU, kinga ya mwili hushuka na kumuweka hatarini kupata magonjwa nyemelezi yanayoweza kusababisha harara inayoambatana na muwasho kwenye ngozi na dalili zingine. Magonjwa hayo ni kama vile;


  • Mambukizi ya molluscum contagiosum- Husababisha harara sehemu yoyote ya mwili.

  • Maambukizi ya kisonono- Husababisha harara kwenye viganja vya mikono na kanyagio

  • Maambukizi ya virusi Herpes- husababisha harara zenye mithiri ya malenge kwenye midomo au uke na ume.

  • Mkanda wa jeshi- Husababishwa na kirusi cha herpes zoster, harara hizi huwa na mwonekano wa malengelenge yenye maumivu makali na husambaa kwenye eneo fulani la ngozi. Hutokea sana usoni na miguuni au kwenye kiwiliwili, hata hivyo huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili.

  • Saratani ya kaposis- Ni aina ya saratani ya ngozi, husababisha harara inayoleta vipele vyenye rangi ya kahawia, zambarau au nyekundu.


Harara kutokana na matumizi ya dawa za ARV


Dawa za kufubaza makali ya VVU baadhi yake zinaweza kusababisha mwitikio wa kinga ya mwili shidi yake na hivyo kuleta harara zinazoambatana na maumivu, vipele au muwasho wa ngozi au mwitikio mkali wa anafailaksia.

Kama una harara na dalili zifuatazo kutokana na matumizi ya ARV onana na daktari haraka;


  • Homa

  • Uchovu

  • Kuvimba ngozi

  • Kuvimba midomo

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya misuli

  • Mvurugiko wa tumbo

  • Kutapika

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuharisha


Dalili hizi humaanisha mwitikio mkali wa kinga ya mwili kwenye dawa.


Dawa za ARV zinazosababisha harara na muwasho wa ngozi

Baadhi ya dawa za ARV zinazoweza kuleta harara na muwasho kwenye ngozi ni;


  • Abacavir (Ziagen)

  • (Epzicom

  • Triumeq

  • Trizivir

  • Raltegravir

  • Dolutegravir

  • Dovato

  • Juluca

  • Triumeq

  • Maraviroc

  • Nevirapine


Matibabu


Matibabu ya harara kwenye ngozi hutegemea kisababishi. Ili kufahamu kisababishi cha harara na muwasho kwenye ngozi yako unapaswa kuwasiliana na daktari kwa uchunguzi.


Matibabu ya nyumbani


Unapaswa kuwasiliana na daktari akushauri kama inafaa kutumia dawa mbadala au dawa za kupunguza muwasho zinazopatikana kwenye maduka ya dawa muhumu bila kuandikiwa cheti cha daktari. Mfano dawa hizo ni zile za kupaka jamii ya antihistamine au hydrocortisone.


Matibabu yasiyo dawa

Ili kuzuia au kuthibiti muwasho wa ngozi kutokana na VVU unaweza kufanya baadhi ya mambo mfano;


  • Kuoga maji ya baridi badala ya maji ya moto

  • Kukaa kivulini na kujiepushe na mwanga mkali wa jua


Makala hii imejibu

  • Je, VVU husabaisha ngozi kuwasha?

  • Je, ngozi kuwasha ni dalili ya VVU?

  • Je, dawa za ARV husababisha muwasho wa ngozi?

  • Je, ufanye nini kutibu muwasho wa ngozi?

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

21 Novemba 2021, 09:08:35

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Roland M. Itchy skin in HIV. Newsline People AIDS Coalit N Y. 1998 Mar:21-5. PMID: 11367452.

2. Altman, et al. “Cutaneous manifestations of human immunodeficiency virus: a clinical update.” Current infectious disease reports vol. 17,3 (2015): 464. doi:10.1007/s11908-015-0464-y

bottom of page