top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Ni dawa jamii ya benzodiazepine inayofanya kazi kwa muda mrefu katika matibabu yamagonjwa ya kutaharuki, wasiwasi na degedege.


Majina ya kibiashara


Majina ya kibiashara ya Clonazepam ni;


  • Clonapam

  • Klonopin

  • Rivotril


Clonazepam ipo kundi gani la dawa?


Clonazepam ni dawa iliyo katika makundi yafuayato;


  • Dawa za wasiwasi

  • Benzodiazepine

  • Dawa za degedege


Dawa zilizo kundi moja na Clonazepam


Dawa zilizo kundi moja na Clonazepam ni;


  • Alparazolam

  • Chlordiazepoxide

  • Diazepam

  • Clobazam

  • Clorazepate

  • Estazolam

  • Flurazepam

  • Lorazepam

  • Midazolam

  • Oxazepam

  • Temazepam

  • Triazolam


Fomu


Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge


Uzito


Kidonge cha Clonazepam huwa na uzito wa;


  • 0.125mg

  • 0.25mg

  • 0.5mg

  • 1mg

  • 2mg


Clonazepam hutibu nini?


  • Degedege

  • Magonjwa ya wasiwasi

  • Kutetemeka mikono na miguu kutokana na wasiwasi

  • Madhaifu ya kukosa usingizi wa REM

  • Sindromu ya mdomo kuungua


Namna inavyofanya kazi


Dawa jamii ya benzodiazepines hufanya mfungamano usio maalumu na risepta ya benzodiazepine BNZ1, inayoshughulika na usingizi na BNZ2, inayoshughulika kulegeza misuli, kusimamisha degedege, kumbukumbu na mjongeo wa kimota. Risepta za benzodiazepine hushirikiana kikazi na risepta gamma-aminobutyric acid-A (GABAA), hii huongeza madhara ya GABA kwa kuongeza uwezo wa GABA kufungamana na risepta GABA. Kufungamana kwa GABA na risepta GABA hufungua njia za chloride na kupunguza mwitikio wa chembe hai.


Ufyozwaji wa dawa


Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika kwenye mfumo wa chakula, kiwango cha dawa kinachoonekana kwenye damu ni hadi 90%% baada ya mtu kumeza na huchukua masaa 1-4 kwa dawa kuanza kuonekana kwenye damu baada ya mtu kumeza.



Mwingiliano wa Clonazepam na chakula


Inaweza kutumika pamoja au bila chakula, hakuna mwingilino uliolipotiwa wa dawa hii endapo itatumika na chakula.


Mwingiliano na pombe


Unapaswa kuepuka pombe wakati unatumia clonazepam kwa kuwa pombe huchochea kuonekana kwa maudhi ya mfumo wa fahamu kama vile kizunguzungu, kuwa kwenye hali ya usingizi mzito, kushindwa fikiria vema, kutoa maamuzi na kuhukumu, kuzimia au kupoteza fahamu. Maudhi mengine ni kushuka haraka kwa mapigo ya upumuaji na mapigo ya moyo.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Clonazepam


  • Wagonjwa wenye mzio wa Clonazepam

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Benzodiazepine


Utoaji taka wa Clonazepam mwilini


Asilimia 50-70 ya clonazepam hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia 10-30 kupitia kinyesi kama mazao ya umetaboli. Kiasi kinachotolewa bila kufanyiwa umetaboli kwenye mkojo ni chini ya asilimia 2 ya dozi iliyotumiwa. Mazao ya umetaboli wa clonazepam kwenye ini ni glucuronide na sulfate


Matumizi ya Clonazepam kwa mama mjamzito


Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliyeko tumboni hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii.


Matumizi ya Clonazepam kwa mama anayenyonyesha


Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inatolewa kwenye maziwa ya mama lakini haijaonesha madhara kwa mtoto hivyo kimoja wapo kinatakiwa kizingatiwe kati ya mama kutumia dawa au mtoto kunyonya.


Dawa zenye muingiliano na Clonazepam


Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Clonazepam;

  • Abametapir

  • Apalutamide

  • Benzhydrocodone/acetaminophen

  • Calcium/magnesium/potassium/sodium oxybates

  • Carbamazepine

  • Conivaptan

  • Fexinidazole

  • Hydrocodone

  • Idelalisib

  • Ivosidenib

  • Lonafarnib

  • Metoclopramide intranasal

  • Selinexor

  • Sodium oxybate

  • Sufentanil sl

  • Tucatinib

  • Valerian

  • Voxelotor


Dawa zinazoweza kutumika na Clonazepam chini ya uangalizi;

  • Amitriptyline

  • Atazanavir

  • Buprenorphine ya kuchoma

  • Butabarbital

  • Chlorpheniramine

  • Chlorpromazine

  • Clarithromycin

  • Clobazam

  • Dextroamphetamine

  • Diazepam

  • Ephedrine

  • Epinephrine

  • Flurazepam

  • Gabapentin

  • Haloperidol

  • Ketamine

  • Ketoconazole

  • Methadone

  • Mifepristone

  • Morphine

  • Phenytoin

  • Pregabalin

  • Rifampin

  • Tramadol

  • Trazodone

  • Triazolam

  • Triclofos

  • Trifluoperazine

  • Trimipramine

  • Triprolidine

  • Voriconazole

  • Xylometazoline

  • Yohimbine

  • Ziconotide

  • Ziprasidone

  • Zotepine


Dawa zenye mwingiliano mdogo Clonazepam;

  • Acetaminophen

  • Acetaminophen iv

  • Acetaminophen rectal

  • Atracurium

  • Biotin

  • Brimonidine

  • Ciprofloxacin

  • Cisatracurium

  • Cyanocobalamin

  • Dexmethylphenidate

  • Esomeprazole

  • Eucalyptus

  • Ezogabine

  • Fleroxacin

  • Gemifloxacin

  • Green tea

  • Levocarnitine

  • Levofloxacin

  • Moxifloxacin

  • Ofloxacin

  • Omeprazole

  • Onabotulinumtoxina

  • Pancuronium

  • Rapacuronium

  • Rifabutin

  • Succinylcholine

  • Valproic acid

  • Vecuronium

  • Vinpocetine

  • Zolpidem


Maudhi madogo ya Clonazepam;


  • Kukosa usawia wa mwili wakati wa kujongea

  • Mwili kuchoka

  • Kusinzia

  • Homa

  • Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji

  • Kutokwa na udenda

  • Maumivu ya kichwa

  • Kupata hasira

  • Mwili kuwasha

  • Kutapika

  • Kukosa usingizi

  • Kikohozi

  • Nimonia

  • Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo

  • Kukosa hamu ya kula

  • Kupata choo kigumu

  • Maumivu wakati wa kumeza

  • Kupoteza kumbukumbu

  • Kupoteza nguvu za kiume



Ufanye nini kama umesahau dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosa

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Clonazepam

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021, 05:14:28

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page