top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Clorazepate ni dawa kundi la benzodiazepine inayotumika kutibu na kuzuia degedege na wasiwasi uliopitiliza.


Majina ya kibiashara ya Clorazepate


Majina mengine ya Clorazepate ni;


  • Tranxene SD

  • Tranxene T-Tabs


Clorazepate ipo kundi gani la dawa?


Clorazepate ipo katika makundi ya dawa yafuatayo;


  • Dawa za wasiwasi

  • Benzodiazepine

  • Dawa za degedege


Dawa zilizo kundi moja na Clorazepate


Dawa zilizo kundi moja na Clorazepate ni;


  • Alparazolam

  • Chlordiazepoxide

  • Diazepam

  • Clobazam

  • Clonazepam

  • Estazolam

  • Flurazepam

  • Lorazepam

  • Midazolam

  • Oxazepam

  • Temazepam

  • Triazolam


Fomu


Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge


Uzito


Kidonge cha Clorazepate kina uzito wa;


  • 3.75mg

  • 7.5mg

  • 15mg


Clorazepate hutibu nini?


  • Ddegedege

  • Wasiwasi

  • Hutibu dalili za kuacha pombe


Namna Clorazepate inavyofanya kazi


Dawa jamii ya benzodiazepines hufanya mfungamano usio maalumu na risepta ya benzodiazepine BNZ1, inayoshughulika na usingizi na BNZ2, inayoshughulika kulegeza misuli, kusimamisha degedege, kumbukumbu na mjongeo wa kimota. Risepta za benzodiazepine hushirikiana kikazi na risepta gamma-aminobutyric acid-A (GABAA), hii huongeza madhara ya GABA kwa kuongeza uwezo wa GABA kufungamana na risepta GABA. Kufungamana kwa GABA na risepta GABA hufungua njia za chloride na kupunguza mwitikio wa chembe hai.


Ufyozwaji wa dawa


Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika kwenye mfumo wa chakula, kiwango cha dawa kinachoonekana kwenye damu hufikia asilimia 91 ya kile kilichomwezwa.


Mwingiliano wa Clorazepate na chakula


Dawa hii inaweza kutumika pamoja au pasipo chakula na hakuna chakula kilichoripotiwa kuwa na mwingiliano na dawa hii kama vitatumika pamoja.


Unaweza kutumia na pombe?


Dawa hii haishauriwi kutumika na pombe yoyote. Matumizi ya Clorazepate na pombe hupelekea kuongezeka kwa dalili za kwenye mfumo wa neva kama vile, kizunguzungu, kuwa kwenye hali ya usingizi mkali, kushindwa tafakari, kuhukumu na kutoa maambuzi sahihi.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Clorazepate


  • Wagonjwa wenye mzio wa Clorazepate

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Benzodiazepine


Utoaji taka wa Clorazepate mwilini


Dawa hii hutolewa nje ya mwili kwa njia ya mkojo.

Matumizi ya Clorazepate kwa mama mjamzito


Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliyeko tumboni hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii.


Matumizi ya Clorazepate kwa mama anayenyonyesha


Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inatolewa kwenye maziwa ya mama lakini haijaonesha madhara kwa mtoto hivyo kimoja wapo kinatakiwa kizingatiwe kati ya mama kutumia dawa au mtoto kunyonya.


Dawa zenye muingiliano na Clorazepate


Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Clorazepate;

  • Abametapir

  • Apalutamide

  • Benzhydrocodone/acetaminophen

  • Calcium/magnesium/potassium/sodium oxybates

  • Conivaptan

  • Enzalutamide

  • Fexinidazole

  • Hydrocodone

  • Idelalisib

  • Ivosidenib

  • Lonafarnib

  • Lopinavir

  • Metoclopramide intranasal

  • Selinexor

  • Sodium oxybate

  • Sufentanil sl

  • Tucatinib

  • Valerian

  • Voxelotor


Dawa zinazoweza kutumika na Clorazepate chini ya uangalizi;


  • Amitriptyline

  • Atazanavir

  • Carbamazepine

  • Clobazam

  • Clonazepam

  • Clonidine

  • Clozapine

  • Diazepam

  • Efavirenz

  • Ephedrine

  • Epinephrine

  • Gabapentin

  • Haloperidol

  • Isoniazid

  • Ketamine

  • Ketoconazole

  • Methadone

  • Morphine

  • Pentobarbital

  • Phenytoin

  • Rifampin

  • Zotepine


Dawa zenye mwingiliano mdogo Clorazepate;


  • Brimonidine

  • Ciprofloxacin

  • Eucalyptus

  • Fleroxacin

  • Gemifloxacin

  • Green tea

  • Levofloxacin

  • Moxifloxacin

  • Ofloxacin

  • Omeprazole

  • Rifabutin

  • Sage

  • Vinpocetine

  • Zolpidem


Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

Maudhi madogo ya Clorazepate;


  • Mwili kuchoka

  • Kusinzia

  • Homa

  • Kizunguzungu

  • Prooling

  • Nervousness

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuchanganyikiwa

  • Maambukizi katika mfumo wa chakula

  • Mdomo kukauka

  • Kutoona v

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Clorazepate

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021, 05:06:25

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page