top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Ethotoin ni moja kati ya dawa inayotumika kuzuia na kupunguza degedege la toniki kloniki na degedege la kutoonekana.


Majina ya kibiashara


Ethotoin hufahamikakwa majina ya kibiashara kama peganone


Ethotoin ipo kundi gani la dawa?


Ethotoin ni dawa iliyo katika kundi la Anticonvulsants na hydantoins.


Dawa zilizo kundi moja


Dawa zilizo kundi moja na Ethotoin ni ;


  • Cerebyx

  • Dilantin

  • Dilantin 125

  • Fosphenytoin

  • Phenytoin

  • Phenytek

  • Sesquient



Fomu


Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge.


Uzito


Ethotoin ina uzito ufuatao;


  • Kidonge

  • 250mg


Ethotoin hutibu nini?


Hutumika kutibu ugonjwa wa degedege la toniki kloniki na complex partial seizure


Namna Ethotoin inavyoweza kufanya kazi


Ethotoin inafanya kazi ya kuzuia na kupunguza degedege kwa mtu mwenye kifafa.


Ufyozwaji wa dawa


Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika kwenye mfumo wa chakula.


Mwingiliano wa Ethotoin na chakula


Dawa hii ni nzuri kutumika mtu akiwa amepata chakula kwani chakula husaidia ufozwaji wa dawa.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ethotoin


  • Wagonjwa wenye mzio wa Ethotoin.

  • Wagonjwa wenye matatizo ya ini.

  • Wagonjwa wenye matatizo ya diskrasias ya damu


Utoaji taka wa Ethotoin mwilini


Dawa hii hutolewa njee kwa njia ya mkojo na haja kubwa.


Matumizi ya Ethotoin kwa mama mjamzito


Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii ina madhara kwa mtoto aliyepo tumboni hivyo itumike palipo na uhitaji mkubwa zaidi wakuokoa maisha ya mama kama hakuna njia mbadala.


Matumizi ya Ethotoin kwa mama anayenyonyesha


Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inatolewa kwenye maziwa ya mama lakini haijaonesha madhara kwa mtoto hivyo hairuhusiwi kwa mama anayenyonyesha.


Dawa zenye mwingiliano na Ethotoin


Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Ethotoin

  • Cyclosporine

  • Dopamine

  • Efavirenz

  • Mebendazole

  • Mestranol

  • Methadone

  • Metoclopramide a ndani ya pua


Dawa zinazoweza kutumika na Ethotoin chini ya uangalizi

  • Amiodarone

  • Amobarbital

  • Brexanolone

  • Busulfan

  • Butabarbital

  • Butalbital

  • Capecitabine

  • Carbamazepine

  • Carboplatin

  • Carmustine

  • Cenobamate

  • Cimetidine

  • Cisplatin

  • Dabigatran

  • Dalteparin

  • Decitabine

  • Deutetrabenazine

  • Disopyramide

  • Disulfiram

  • Docetaxel

  • Doxorubicin

  • Doxorubicin liposomal

  • Fluconazole

  • Fluorouracil

  • Fluoxetine

  • Fluvoxamine

  • Fondaparinux

  • Gemifloxacin

  • Heparin

  • Imatinib

  • Ketoconazole

  • Metronidazole

  • Metyrapone

  • Mexiletine

  • Miconazole a ukeni

  • Moxifloxacin

  • Phenobarbital

  • Posaconazole

  • Primidone

  • Protamine

  • Quinidine

  • Rifampin

  • Sulfamethoxazole

  • Voriconazole

  • Warfarin


Dawa zenye mwingiliano mdogo Ethotoin

  • Acetazolamide

  • Auranofin

  • Brinzolamide

  • Carbamazepine

  • Caspofungin

  • Chloramphenicol

  • Clopidogrel

  • Diazoxide

  • Disulfiram

  • Doxycycline

  • Ethanol

  • Ethosuximide

  • Felbamate

  • Folic acid

  • Furosemide

  • Lithium

  • Meperidine

  • Methazolamide

  • Methsuximide

  • Oxcarbazepine

  • Phenobarbital

  • Pyridoxine

  • Pyridoxine (Kiua sumu)

  • Pyrimethamine

  • Rifabutin

  • Sucralfate

  • Sulfadiazine

  • Sulfamethoxazole

  • Sulfisoxazole

  • Thyroid desiccated

  • Tiagabine

  • Tibolone

  • Tolazamide

  • Tolbutamide

  • Topiramate

  • Trazodone

  • Valproic acid

  • Vigabatrin

  • voriconazole


Maudhi madogo ya Ethotoin


  • Mwili kuchoka

  • Kushindwa kulala vizuri

  • Homa

  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kichwa

  • Huzuniko

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kuharisha

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Ataxia

  • Kuchanganyikiwa

  • Maumivu ya kifua

  • Kupata ganzi

  • Sindromu ya stevens Johnson

  • Diplopia


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Ni muhimu kutumia dozi kwa wakati sahihi, kama umesahau kutumia dozi yako wasiliana na daktari au mfamasia wako akupe maelekezo sahihi ya kutumia dozi inayofuata.

13 Juni 2023 19:18:46

Dawa Ethotoin

Imeboreshwa,

30 Oktoba 2021 18:55:12

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.

  2. Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.

  3. Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.

  4. Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537. 

  5. DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.

  6. Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.

  7. Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.

  8. Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277. 

  9. Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29. 

  10. Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.

  11. Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.

bottom of page