top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Hydralazine ni moja kati ya dawa inayotumika kushusha shinikizo la juu la damu na kuzuia magonjwa kama kiharusi, magonjwa ya moyo na figo. Inafanya kazi kwa kutanua mishipa ya damu.


Majina mengine ya Hydralazine


Majina mengine ya Hydralazine ni;


  • Apresoline

  • Bidil


Hydralazine ipo kundi gani la dawa?


Hydralazine ni dawa iliyo katika kundi la Vasodilators.


Dawa zilizo kundi moja na Hydralazine


Dawa zilizo kundi moja na Hydralazine ni ;


  • Nitrogycerin

  • Isosorbide mononitrate

  • Isosorbide dinitrate

  • Minoxidil

  • Fenoldopam

  • Nitroprusside


Fomu ya dawa ya Hydralazine


Dawa hii ipo katika fomu ya;


  • Solusheni kwaajiri ya sindano

  • Kidonge


Uzito wa dawa ya Hydralazine


Hydralazine ina uzito ufuatao;


Solusheni kwaajiri ya sindano


  • 20mg/ml


Vidonge


  • 10mg

  • 25mg

  • 50mg

  • 100mg


Hydralazine hutibu nini?


Hutumika kutibu shinikizo la damu iliyo juu


  • Hutumika kutibu shinikizo la damu kwa wajawazito (Eclampsia)

  • Hutumika kutibu congestive heart failure


Namna Hydralazine inavyoweza kufanya kazi


Hydralazine inapoingia kwenye damu hufanya kazi ya kupanua mishipa ya damu moja kwa moja hasa kwenye ateri na veini kidogo hivyo kupunguza shinikizo la damu na kufanya damu izunguke vizuri mwilini.


Ufyozwaji wa dawa


Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ikitumika na chakula kwani chakula husaidia Kiwango cha dawa kinachoingia kwenye damu baada ya mtu kumeza dawa.


Mwingiliano wa Hydralazine na chakula


Dawa hii ni nzuri kutumika mtu akiwa amepata chakula kwani chakula husaidia katika ufyozwaji wa dawa.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Hydralazine


  • Wagonjwa wenye mzio wa Hydralazine.

  • Wagonjwa wenye coronary artery disease.

  • Wagonjwa wenye mitral valvular rheumatic heart disease.


Utoaji taka wa Hydralazine mwilini


Asilimia kumi na nne (14%) ya dawa ambayo haijabadirishwa hutolewa kwa njia ya mkojo.


Matumizi ya Hydralazine kwa mama mjamzito


Tafiti zinaonesha kuwa tahadhari inatakiwa wakati mama mjamzito anatumia dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto aliye tumboni kwa mama.


Matumizi ya Hydralazine mama anayenyonyesha


Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inatolewa njee kupitia maziwa ya mama hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anayeyonyesha anapotumia dawa hii.


Dawa zenye muingiliano na Hydralazine


Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Hydralazine;

  • Lofexidine

  • Lonafarnib

  • Pexidartinib

  • Pretomanid


Dawa zinazoweza kutumika na Hydralazine chini ya uangalizi;

  • Acebutolol

  • Aceclofenac

  • Acemetacin

  • Aldesleukin

  • Amifostine

  • Aspirin

  • Aspirin rectal

  • Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate

  • Atenolol

  • Avanafil

  • Axitinib

  • Benzphetamine

  • Betaxolol

  • Bisoprolol

  • Bretylium

  • Carbidopa

  • Carvedilol

  • Celecoxib

  • Choline magnesium trisalicylate

  • Dexfenfluramine

  • Dexmethylphenidate

  • Dextroamphetamine

  • Diclofenac

  • Diethylpropion

  • Diflunisal

  • Dobutamine

  • Dopamine

  • Ephedrine

  • Epinephrine

  • Epoprostenol

  • Esmolol

  • Etodolac

  • Fenfluramine

  • Fenoldopam

  • Fenoprofen

  • Finerenone

  • Flibanserin

  • Flurbiprofen

  • Ibuprofen

  • Ibuprofen iv

  • Iloprost

  • Indomethacin

  • Labetalol

  • Lemborexant

  • Levodopa

  • Linezolid

  • Meclofenamate

  • Mefenamic acid

  • Meloxicam

  • Nabumetone

  • Phenylephrine

  • Procarbazine

  • Propranolol

  • Sulfasalazine

  • Tazemetostat

  • Timolol

  • Tinidazole

  • Tolfenamic acid


Dawa zenye mwingiliano mdogo na Hydralazine;

  • Agrimony

  • Brimonidine

  • Celiprolol

  • Cornsilk

  • Diazoxide

  • Forskolin

  • Maitake

  • Pyridoxine

  • Pyridoxine (antidote)

  • Reishi

  • Ruxolitinib

  • Shepherd's purse

  • Tizanidine

  • Treprostinil


Maudhi madogo ya Hydralazine

  • Shinikizo la damu kuwa chini

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya kichwa

  • Palpitation

  • Macho kutoa uchafu na kuwa mekundu

  • Kichefuchefu

  • Mapigo ya moyo kuwa juu

  • Mwili kuvimba

  • Vascular collapse

  • Peripheral neuropathy

  • Kukosa hamu ya kula

  • Kuharisha

  • Kutapika

  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kifua

  • Kushindwa kupumua

  • Leukopenia

  • Nasal congestion

  • Rheumatoid arthritis

  • Agranulocytosis

  • Mwili kuchoka

  • Maumivu wakati wa kukojoa au kushindwa kukojoa


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa hydralazine

Imeboreshwa,

29 Oktoba 2021, 15:36:29

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page