Mwandishi:
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
Iloprost ni moja kati ya dawa inayotumika kutibu shinikizo la damu la juu la damu kwenye mapafu.
Majina ya kibiashara
Majina ya kibiashara ya Iloprost ni;
Ventavis
Iloprost ipo kundi gani la dawa?
Iloprost ni dawa iliyo katika kundi la Prostacyclin analogs.
Dawa zilizo kundi moja na Iloprost
Dawa zilizo kundi moja na Iloprost ni ;
Epoprostenol
Treprostinil
Fomu ya dawa ya Iloprost
Dawa hii ipo katika fomu ya;
Ampule ya kutumia mara moja (single use ampule)
Uzito wa dawa ya Iloprost
Iloprost ina uzito ufuatao;
Ampule ya kutumia mara moja
10mcg/ml (1ml)
20mcg/ml (1ml)
Iloprost hutibu nini?
Hutumika kutibu shinikizo la damu (pressure) iliyojuu kwenye mapafu (pulmonary arterial hypertension)
Namna Iloprost inavyoweza kufanya kazi
Prostaglandins zinapatikana kwenye tishu na majimaji ya mwilini na kupatanisha kazi za mwili. Iloprost ni moja wapo katika familia ya prostaglandins ambazo hutoka kwenye arachidonic acid. Kazi kubwa ya Iloprost ni kuzuia mkusanyiko wa platelet.
Ufyozwaji wa dawa
Kiwango cha dawa kinachoingia kwenye damu baada ya mtu kumeza dawa ni 63% na ufozwaji wake ufanyika haraka.
Mwingiliano wa Iloprost na chakula
Dawa hii inaweza kutumika mtu akiwa amepata chakula au akiwa hajapata chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Iloprost
Wagonjwa wenye mzio wa Iloprost.
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya prostacyclin analogs.
Utoaji taka wa Iloprost mwilini
Asilimia sitini na nane (68%) ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia kumi na mbili (12%) hutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Matumizi ya Iloprost kwa mama mjamzito
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito na mtoto aliye tumboni hivyo taadhari inatakiwa kuchukuliwa wakati mama anatumia dawa hii.
Matumizi ya Iloprost mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo kimoja wapo kati ya mtoto kunyonya na mama kutumia dawa inatakiwa viangaliwe kulingana na uhitaji .
Dawa zenye muingiliano na Iloprost
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Iloprost
Lofexidine
Dawa zinazoweza kutumika na Iloprost chini ya uangalizi
Aldesleukin
Amifostine
Benazepril
Captopril
Carbidopa
Dabigatran
Eluxadoline
Epoprostenol
Fenoldopam
Fish oil triglycerides
Hydralazine
Ibrutinib
Levodopa
Minoxidil
Treprostinil
Xipamide
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Iloprost
Agrimony
Brimonidine
Cornsilk
Forskolin
Maitake
Octacosanol
Reishi
Shepherd's purse
Tizanidine
Treprostinil
Maudhi madogo ya Iloprost
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Maumivu ya kichwa
Taya kuuma
Flushing
Maumivu ya misuli
Kichefuchefu
Maumivu ya mgongo
Syncope
Kukosa usingizi
Trismus
Shinikizo la damu kuwa chini
Mapigo ya moyo kuwa juu
Nimonia
Maumivu ya ulimi
Misuli kukaza
Hemoptysis
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
17 Januari 2026, 15:31:06
Dawa Iloprost
Imeboreshwa,
29 Oktoba 2021, 14:03:01
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.
Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.
McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.
World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.
Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].
Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.
