top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Isosorbide dinitrate ni moja kati ya dawa inayotumika kutibu na kuzuia maumivu ya kifua (Angina) kwa wagonjwa wenye magonjwa ya moyo.


Majina mengine ya Isosorbide dinitrate


Majina mengine ya Isosorbide dinitrate ni;


  • Dilatrate-SR

  • Isordil

  • Isordil titradose

  • ISDN

  • Bidil

  • Isochron

  • IsoDitrate

  • Apo-Isdn


Isosorbide dinitrate ipo kundi gani la dawa?


Isosorbide dinitrate ni dawa iliyo katika kundi la Nitrates, Angina.


Dawa zilizo kundi moja na Isosorbide dinitrate


Dawa zilizo kundi moja na Isosorbide dinitrate ni ;


  • Nitrogycerin

  • Hydralazine

  • Isosorbide mononitrate

  • Minoxidil

  • Fenoldopam

  • Nitroprusside


Fomu ya dawa ya Isosorbide dinitrate


Dawa hii ipo katika fomu ya;


  • Kidonge

  • Tembe


Uzito wa dawa ya Isosorbide dinitrate


Isosorbide dinitrate ina uzito ufuatao;


Vidonge/Tembe (tablets extended release)


  • 40mg


Vidonge vya kutumia chini ya ulimi (sublingual)


  • 2.5mg

  • 5mg


Vidonge


  • 5mg

  • 10mg

  • 20mg

  • 30mg

  • 40mg


Isosorbide dinitrate hutibu nini?


  • Hutumika kutibu Angina pectoris.


Namna Isosorbide dinitrate inavyoweza kufanya kazi


Isosorbide dinitrate inapoingia kwenye damu hufanya kazi ya kupanua mishipa ya damu moja kwa moja hasa kwenye ateri na veini kidogo hivyo kupunguza shinikizo la damu na kufanya damu izunguke vizuri mwilini.


Ufyozwaji wa dawa


Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula. Kiwango cha dawa kinachoingia kwenye damu kwa haraka ni 40%-50%.



Mwingiliano wa Isosorbide dinitrate na chakula


Dawa hii ni nzuri ikutumika nusu saa kabla ya kula au saa moja baada ya kula chakula.



Wagonjwa wasiopaswa kutumia Isosorbide dinitrate


  • Wagonjwa wenye mzio wa Isosorbide dinitrate.

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Nitrates.


Utoaji taka wa Isosorbide dinitrate mwilini


Asilimia themanini hadi mia moja (80%-100%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo lakini pia hutolewa kwa njia ya haja kubwa.


Matumizi ya Isosorbide dinitrate kwa mama mjamzito


Tafiti zinaonesha kuwa tahadhari inatakiwa wakati mama mjamzito anatumia dawa hii kwani inaweza kuleta madhara kwa mtoto aliye tumboni kwa mama.


Matumizi ya Isosorbide dinitrate mama anayenyonyesha


Hakuna tafiti zinazoonesha kama dawa hii inasambaa kwenye maziwa ya mama, ina madhara ya mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii.


Dawa zenye muingiliano na Isosorbide dinitrate



Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Isosorbide dinitrate;

  • Abametapir

  • Apalutamide

  • Cabergoline

  • Carbamazepine

  • Ergotamine

  • Fexinidazole

  • Fosphenytoin

  • Idelalisib

  • Ivosidenib

  • Lofexidine

  • Methylergonovine

  • Phenobarbital

  • Phenytoin

  • Tucatinib

  • Voxelotor


Dawa zinazoweza kutumika na Isosorbide dinitrate chini ya uangalizi;

  • Arginine

  • Belzutifan

  • Benazepril

  • Bosentan

  • Bretylium

  • Bupivacaine implant

  • Captopril

  • Cenobamate

  • Conivaptan

  • Crofelemer

  • Dabrafenib

  • Dapsone topical

  • Duvelisib

  • Efavirenz

  • Elagolix

  • Elvitegravir/cobicistat/emtricitabine/tenofovir df

  • Encorafenib

  • Etravirine

  • Fedratinib

  • Iloperidone

  • Istradefylline

  • Lorlatinib

  • Maraviroc

  • Mitotane

  • Nafcillin

  • Nitroglycerin rectal

  • Primidone

  • Ribociclib

  • Rifabutin

  • Rucaparib

  • Stiripentol

  • Tazemetostat

  • Tecovirimat

  • Tetracaine


Dawa zenye mwingiliano mdogo na Isosorbide dinitrate;

  • Acetylcysteine (Antidote)

  • Rifampin

  • Rifapentine


Maudhi madogo ya Isosorbide dinitrate


  • Shinikizo la damu kuwa chini

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya kichwa

  • Palpitation

  • Mapigo ya moyo kuwa juu

  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kifua

  • Kushindwa kupumua

  • Mwili kuchoka

  • Syncope

  • Rebound hypertension

  • Unstable angina flushing

  • Methemoglobinemia


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka kama muda wa dozi uliyosahau ni ndani ya masaa mawili kufika dozi inayofuata usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Isosorbide dinitrate

Imeboreshwa,

29 Oktoba 2021, 13:56:35

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page