top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamina L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Isosorbide mononitrate ni moja kati ya dawa inayotumika kutibu na kuzuia maumivu ya kifua (Angina) kwa wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu ya koronari.


Majina ya kibiashara


Majina kibiashara ya Isosorbide mononitrate ni pamoja na;


  • Imolur

  • Monoket

  • ISMO


Isosorbide mononitrate ipo kundi gani la dawa?


Isosorbide mononitrate ni dawa iliyo katika kundi la Nitrates, Angina.


Dawa zilizo kundi moja na Isosorbide mononitrate


Dawa zilizo kundi moja na Isosorbide mononitrate ni ;


  • Nitrogycerin

  • Hydralazine

  • Isosorbide dinitrate

  • Minoxidil

  • Fenoldopam

  • Nitroprusside


Fomu ya dawa ya Isosorbide mononitrate


Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge


Uzito wa dawa ya Isosorbide mononitrate


Isosorbide mononitrate ina uzito ufuatao;


Vidonge


  • 10mg

  • 20mg


Vidonge ( vinavyofanya kazi muda mrefu)


  • 30mg

  • 60mg

  • 120mg


Isosorbide mononitrate hutibu nini?


Hutumika kutibu Angina pectoris.


Namna Isosorbide mononitrate inavyoweza kufanya kazi


Isosorbide mononitrate inapoingia kwenye damu hufanya kazi ya kupanua mishipa ya damu moja kwa moja hasa kwenye ateri na veini kidogo hivyo kupunguza shinikizo la damu na kufanya damu izunguke vizuri mwilini.


Ufyozwaji wa dawa


Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula itumike nusu saa kabla mtu hajapata chakula au saa moja baada ya kula.


Mwingiliano wa Isosorbide mononitrate na chakula


Dawa hii ni nzuri ikutumika nusu saa kabla ya kula au saa moja baada ya kula chakula.



Wagonjwa wasiopaswa kutumia Isosorbide mononitrate


  • Wagonjwa wenye mzio wa Isosorbide mononitrate.

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Nitrates.


Utoaji taka wa Isosorbide mononitrate mwilini


Asilimia mbili (2%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia moja (1%) ya dawa hutolewa kwa njia ya haja kubwa.


Matumizi ya Isosorbide mononitrate kwa mama mjamzito


Tafiti zinaonesha kuwa tahadhari inatakiwa wakati mama mjamzito anatumia dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto aliye tumboni kwa mama.


Matumizi ya Isosorbide mononitrate mama anayenyonyesha


Hakuna tafiti zinazoonesha kama dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama, ina madhara ya mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii.


Dawa zenye muingiliano na Isosorbide mononitrate



Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Isosorbide mononitrate;

  • Abametapir

  • Apalutamide

  • Cabergoline

  • Carbamazepine

  • Ergoloid mesylates

  • Ergotamine

  • Fexinidazole

  • Fosphenytoin

  • Idelalisib

  • Ivosidenib

  • Lofexidine

  • Methylergonovine

  • Phenobarbital

  • Phenytoin

  • Tucatinib

  • Voxelotor


Dawa zinazoweza kutumika na Isosorbide mononitrate chini ya uangalizi;

  • Arginine

  • Belzutifan

  • Bosentan

  • Bretylium

  • Bupivacaine implant

  • Captopril

  • Cenobamate

  • Conivaptan

  • Crofelemer

  • Dabrafenib

  • Dapsone topical

  • Dichlorphenamide

  • Duvelisib

  • Efavirenz

  • Elagolix

  • Elvitegravir/cobicistat/emtricitabine/tenofovir df

  • Encorafenib

  • Etravirine

  • Fedratinib

  • Iloperidone

  • Istradefylline

  • Lorlatinib

  • Maraviroc

  • Mitotane

  • Nafcillin

  • Nitroglycerin rectal

  • Primidone

  • Ribociclib

  • Rifabutin

  • Rucaparib

  • Stiripentol

  • Tazemetostat

  • Tecovirimat

  • Tetracaine


Dawa zenye mwingiliano mdogo na Isosorbide mononitrate;

  • Acetyl cysteine (Antidote)

  • Rifampin

  • Rifapentine


Maudhi madogo ya Isosorbide mononitrate;


  • Shinikizo la damu kuwa chini

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya kichwa

  • Palpitation

  • Macho kutoa uchafu na kuwa mekundu

  • Kichefuchefu

  • Mapigo ya moyo kuwa juu

  • Mwili kuvimba

  • Vascular collapse

  • Peripheral neuropathy

  • Kukosa hamu ya kula

  • Kuharisha

  • Kutapika

  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kifua

  • Kushindwa kupumua

  • Mwili kuchoka


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka kama muda wa dozi uliyosahau ni ndani ya masaa sita, ila kama umesahau zaidi ya masaa sita usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Isosorbide mononitrate

Imeboreshwa,

29 Oktoba 2021, 13:56:15

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page