Mwandishi:
Dkt. mercy M, CO
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
Minoxidil ni moja kati ya dawa inayotumika kutibu magonjwa ya shinikizo la juu la damuna hivyo kuzuia magonjwa kama kiharusi, magonjwa ya moyo na figo. Inafanya kazi kwa kupanua mishipa ya damu na hivyo kupuguza shinikizo lililo ndnai yake.
Majina ya kibiashara
Majina yak ibiashara ya Minoxidil ni;
Loniten
Minodyl
Minoxidil HTN
Minoxidil ipo kundi gani la dawa?
Minoxidil ni dawa iliyo katika kundi la Vasodilators.
Dawa zilizo kundi moja na Minoxidil
Dawa zilizo kundi moja na Minoxidil ni ;
Nitrogycerin
Isosorbide mononitrate
Isosorbide dinitrate
Hydralazine
Fenoldopam
Nitroprusside
Fomu ya dawa ya Minoxidil
Dawa hii ipo katika fomu yay a kidonge
Uzito wa dawa ya Minoxidil
Kidonge huwa na uzito wa 2.5mg au 10mg
Minoxidil hutibu nini?
Hutumika kutibu shinikizo la damu iliyo juu (Severe or Refractory Hypertension)
Namna Minoxidil inavyoweza kufanya kazi
Minoxidil inapoingia kwenye damu hufanya kazi ya kupanua mishipa ya damu moja kwa moja hasa kwenye ateri na veini kidogo hivyo kupunguza shinikizo la damu na kufanya damu izunguke vizuri mwilini.
Ufyozwaji wa dawa
Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula na kiwango cha dawa kinachopatikana kwenye damu baada ya mtu kutumia ni 90% na huanza kuonekana ndani ya saa moja baada ya mtu kumeza dawa.
Mwingiliano wa Minoxidil na chakula
Dawa hii inaweza kutumika mtu akiwa amepata chakula au akiwa hajapata chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Minoxidil
Wagonjwa wenye mzio wa Minoxidil
Wagonjwa wenye Pheochromocytoma
Utoaji taka wa Minoxidil mwilini
Asilimia kumi na mbili (12%) ya dawa ambayo haijabadirishwa hutolewa kwa njia ya mkojo.
Matumizi ya Minoxidil kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa tahadhari inatakiwa wakati mama mjamzito anatumia dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto aliye tumboni kwa mama.
Matumizi ya Minoxidil kwa mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inatolewa njee kupitia maziwa ya mama hivyo hairuhusiwi kwa matumizi ya muda mrefu kwa mama anayenyonysha.
Dawa zenye muingiliano na Minoxidil
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Minoxidil;
Bremelanotide
Lofexidine
Dawa zinazoweza kutumika na Minoxidil chini ya uangalizi;
Aldesleukin
Amifostine
Avanafil
Bretylium
Carbidopa
Dulaglutide
Epoprostenol
Fenoldopam
Ferric maltol
Hydralazine
Iloprost
Levodopa
Maraviroc
Nitroglycerin rectal
Tadalafil
Teduglutide
Treprostinil
Xipamide
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Minoxidil;
Agrimony
Amiloride
Bendroflumethiazide
Brimonidine
Bumetanide
Chlorothiazide
Chlorthalidone
Cornsilk
Cyclopenthiazide
Drospirenone
Ethacrynic acid
Forskolin
Furosemide
Hydrochlorothiazide
Indapamide
Maitake
Methyclothiazide
Metolazone
Reishi
Spironolactone
Tizanidine
Torsemide
Treprostinil
Triamterene
Maudhi madogo ya Minoxidil
Shinikizo la damu kuwa chini
Maumivu ya kichwa
Palpitation
Mapigo ya moyo kuwa juu
Mwili kuota nywele
ECG kuwa tofauti
Pericardial effusion
Kizunguzungu
Maumivu ya kifua
Kushindwa kupumua
Fluid and sodium retention
Pericarditis
Steven Johnson syndrome
Hirsutism
Leukopenia
Thrombocytopenia
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
13 Juni 2023 19:18:46
Dawa minoxidil
Imeboreshwa,
29 Oktoba 2021 15:23:59
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.
Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.
Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.
Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537.
DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.
Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.
Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.
Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277.
Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29.
Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.
Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.