top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Sildenafil ni moja kati ya dawa inayotumika kutibu matatizo ya kushindwa kusimamisha uume au kusimamisha kwa muda mfupi na kushusha shinikizo la la juu la damu kwenys mapafudamu iliyojuu kwenye mapafu.


Majina ya kibiashara


Majina mengine ya kibiashara ya sildenafil ni;


  • Revatio

  • Viagra


Sildenafil ipo kundi gani la dawa?


Sildenafil ni dawa iliyo katika kundi la PAH, PDE-5 Inhibitors; Phosphodiesterase-5 Enzyme Inhibitors.


Dawa zilizo kundi moja na Sildenafil


Dawa zilizo kundi moja na Sildenafil ni ;


  • Vardenafil

  • Tadalafil

  • Avanafil


Fomu ya Sildenafil


Dawa hii ipo katika fomu ya;


  • Kidonge

  • Solusheni kwaajiri ya sindano

  • Solusheni kwaajiri ya kunywa


Uzito wa Sildenafil


Sildenafil ina uzito ufuatao;


Vidonge (Revatio)


  • 20mg


Vidonge (Viagra)


  • 25mg

  • 50mg

  • 100mg


Solusheni kwaajiri ya sindano


  • 10mg/12.5ml


Kimiminika cha kunywa


  • 10mg/ml


Sildenafil hutibu nini?


  • Hutumika kutibu matatizo kwa wanaume wasio na uwezo wa kusimamisha uume kwa muda mrefu

  • Hutumika kutibu shinikizo la damu iliyojuu kwenye mapafu.


Namna Sildenafil inavyoweza kufanya kazi


Sildenafil hufanya kazi ya kuzuia PDE-5 hivyo kuongeza cyclic guanosine monophosphate cGMP na kuruhusu mishipa iweze kutanuka.





Ufyozwaji wa dawa


Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula, kiwango cha dawa kinachoonekana kwenye damu baada ya kutumia ni 40% na huanza kuonekana kwenye damu ndani ya dakika 30-120 baada ya mtu kumeza dawa.


Mwingiliano wa Sildenafil na chakula


Dawa hii inaweza kutumika mtu akiwa amepata chakula au akiwa hajapata chakula.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Sildenafil


  • Wagonjwa wenye mzio wa Sildenafil.

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya PDE-5 Inhibitors; Phosphodiesterase-5 Enzyme inhibitors.


Utoaji taka wa Saldenafil mwilini


Asilimia themanini (80%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya haja kubwa na asilimia kumi na tatu (13%) hutolewa kwa njia ya mkojo.


Matumizi ya Sildenafil kwa mama mjamzito


Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito lakini mwanamke mwenye matatizo ya moyo asipotibiwa anaweza anakuwa kwenye hatari ya kujifungua kabla ya muda pia mama kuwa kwenye hatari ya kifo.


Matumizi ya Sildenafil kwa mama anayenyonyesha


Hakuna tafiti zinazoonesha kuwa dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mama anayenyonysha, kwa mtoto anayenyosha na katika uzalishwaji wa maziwa.


Dawa zenye muingiliano na Sildenafil



Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Sildenafil

  • Abametapir

  • Alfuzosin

  • Amyl nitrite

  • Apalutamide

  • Asenapine

  • Chloramphenicol

  • Clarithromycin

  • Conivaptan

  • Crizotinib

  • Dabrafenib

  • Doxazosin

  • Eslicarbazepine acetate

  • Fexinidazole

  • Glyceryl trinitrate pr

  • Ivosidenib

  • Ketoconazole

  • Lonafarnib

  • Lopinavir

  • Mifepristone

  • Mitotane

  • Nafcillin

  • Ombitasvir/paritaprevir/ritonavir & dasabuvir

  • Oxcarbazepine

  • Pentobarbital

  • Phenobarbital

  • Phenoxybenzamine

  • Phentolamine

  • Phenytoin

  • Prazosin

  • Primidone

  • Ritonavir

  • Silodosin

  • St john's wort

  • Terazosin

  • Tucatinib

  • Voxelotor


Dawa zinazoweza kutumika na Sildenafil chini ya uangalizi

  • Acebutolol

  • Amifostine

  • Artemether/lumefantrine

  • Atenolol

  • Benazepril

  • Captopril

  • Carbamazepine

  • Carvedilol

  • Cenobamate

  • Cimetidine

  • Cyclosporine

  • Darunavir

  • Deferasirox

  • Dexamethasone

  • Efavirenz

  • Epoprostenol

  • Erythromycin base

  • Griseofulvin

  • Idelalisib

  • Iloperidone

  • Indinavir

  • Isoniazid

  • Istradefylline

  • Itraconazole

  • Labetalol

  • Lapatinib

  • Lesinurad

  • Letermovir

  • Levamlodipine

  • Lorlatinib

  • Maraviroc

  • Metoprolol

  • Miconazole vaginal

  • Nebivolol

  • Nefazodone

  • Nevirapine

  • Nifedipine

  • Nilotinib

  • Nitroprusside sodium

  • Penbutolol

  • Pindolol

  • Posaconazole

  • Propranolol

  • Ribociclib

  • Rifabutin

  • Rifampin

  • Voriconazole


Dawa zenye mwingiliano mdogo na Sildenafil;

  • Labetalol

  • Macitentan

  • Sapropterin


Maudhi madogo ya Sildenafil


  • Maumivu ya kichwa

  • kichefuchefu

  • Kutokwa na jasho

  • Kukosa usingizi

  • Kutokwa damu puani

  • Kiungulia

  • Kizunguzungu

  • Wekundu kwenyengozi

  • Kuharisha

  • kizunguzungu

  • Vipele kwenye ngozi


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi.Kama umesahau kutumia dozi yako kwa wakati sahihi wasiliana na daktari wako au mfamasia akupe maelekezo ya dozi inayofuata.


17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Sildenafil

Imeboreshwa,

30 Oktoba 2021, 18:29:27

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page