Mwandishi:
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Tetrabenazine ni moja kati ya dawa inayotumika kupunguza miondoko isiyokuwa ya kawaida (chorea) inayosababishwa na magonjwa ya huntington.
Majina mengine ya Tetrabenazine
Majina mengine ya Tetrabenazine ni;
Xenazine
Nitoman
Tetrabenazine ipo kundi gani la dawa?
Tetrabanazine ni dawa iliyo katika kundi la VMAT2 Inhibitors.
Dawa zilizo kundi moja na Tetrabenazine
Dawa zilizo kundi moja na Tetrabenazine ni;
Deutetrabenazine
Valbenazine
Fomu ya dawa ya Tetrabenazine
Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge
Uzito wa dawa ya Tetrabenazine
Tetrabenazine ina uzito ufuatao;
Vidonge
12.5mg
25mg
Tetrabenazine hutibu nini?
Hutumika kutibu ugonjwa wa huntington.
Namna Tetrabenazine inavyoweza kufanya kazi
Tetrabenazine hufanya kazi kwa kuzuia human vesicular monoamine transporter type 2 (VMAT2) hivyo kupunguza monoamines inayozalishwa kwenye nevu ya synaptic na depletion ya monoamine stores kutoka kwenye nevu.
Ufyozwaji wa dawa
Ufyozwaji wa dawa hii hufanyika kwenye mfumo wa chakula hadi asilimia sabini na tano.
Mwingiliano wa Tetrabenazine na chakula
Dawa hii inaweza kutumika mtu akiwa amepata chakula au akiwa hajapata chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Tetrabenazine
Wagonjwa wenye mzio wa Tetrabenazine.
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya VMAT2 Inhibitors.
Utoaji taka wa Tetrabenazine mwilini
Asilimia sabini na tano (75%) ya Dawa hii hutolewa njee kwa njia ya mkojo na asilimia saba hadi kumi na sita (7%-16%) hutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Matumizi ya Tetrabenazine kwa mama mjamzito
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliyeko tumboni hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii.
Matumizi ya Tetrabenazine kwa mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha kuwa dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mama anayenyonysha, kwa mtoto anayenyosha na katika uzalishwaji wa maziwa. Hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii.
Dawa zenye muingiliano na Tetrabenazine
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Tetrabenazine;
Alfuzosin
Apomorphine
Aripiprazole
Artemether
Atomoxetine
Bedaquiline
Ceritinib
Dofetilide
Encorafenib
Entrectinib
Eribulin
Escitalopram
Fexinidazole
Glasdegib
Histrelin
Hydroxychloroquine sulfate
Inotuzumab
Iobenguane i 131
Lefamulin
Mefloquine
Metoclopramide intranasal
Panobinostat
Pimavanserin
Pitolisant
Ribociclib
Safinamide
Triptorelin
Dawa zinazoweza kutumika na Tetrabenazine chini ya uangalizi;
Abiraterone
Albuterol
Alfuzosin
Amoxapine
Arformoterol
Aripiprazole
Brexanolone
Cenobamate
Chlorpromazine
Ciprofloxacin
Clobazam
Clozapine
Fluoxetine
Fluphenazine
Fostemsavir
Haloperidol
Iloperidone
Lasmiditan
Lemborexant
Lenvatinib
Lofexidine
Metoclopramide
Paliperidone
Paroxetine
Perphenazine
Pimozide
Prochlorperazine
Promethazine
Quetiapine
Quinidine
Remimazolam
Risperidone
Ritonavir
Selpercatinib
Stiripentol
Thioridazine
Thiothixene
Triclabendazole
Trifluoperazine
Voclosporin
Ziprasidone
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Tetrabenazine;
Azithromycin
Chloroquine
Maudhi madogo ya Tetrabenazine;
Inaleta usingizi
Mwili kuchoka
Kukosa usingizi
Msongo wa mawazo
Akathisia
kutapika
Kukosa hamu ya kula
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Extrapyramidal events
Kupata woga
Kichefuchefu
Bruising
Maumivu wakati wa kukojoa
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
17 Januari 2026, 15:31:06
Dawa Tetrabenazine
Imeboreshwa,
29 Oktoba 2021, 13:56:57
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.
Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.
McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.
World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.
Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].
Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.
