top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Treprostinil ni moja kati ya dawa inayotumika kushusha shinikizo la juu la dmau kwenye mapafu.


Majina mengine ya Treprostinil


Majina mengine ya Treprostinil ni;


  • Remodulin

  • Orenitram

  • Tyvaso


Treprostinil ipo kundi gani la dawa?


Treprostinil ni dawa iliyo katika kundi la Prostacyclin analogs.


Dawa zilizo kundi moja na Treprostinil


Dawa zilizo kundi moja na Treprostinil ni ;


  • Epoprostenol

  • Iloprost


Fomu ya dawa ya Treprostinil


Dawa hii ipo katika fomu ya;


  • Solusheni kwaajiri ya sindano

  • Kidonge


Uzito wa dawa ya Treprostinil


Treprostinil ina uzito ufuatao;


Solusheni kwaajiri ya sindano


  • 1mg/ml

  • 2.5mg/ml

  • 5mg/ml

  • 10mg/ml


Vidonge


  • 0.125mg

  • 0.25mg

  • 2.5mg

  • 5mg


Treprostinil hutibu nini?


Hutumika kutibu shinikizo la damu (pressure) iliyojuu kwenye mapafu (pulmonary arterial hypertension)


Namna Treprostinil inavyoweza kufanya kazi


Prostaglandins zinapatikana kwenye tishu na majimaji ya mwilini na kupatanisha kazi za mwili. Treprostinil ni moja wapo katika familia ya prostaglandins ambazo hutoka kwenye arachidonic acid. Kazi kubwa ya Treprostinil ni kuzuia mkusanyiko wa platelet.


Ufyozwaji wa dawa


Kiwango cha dawa kinachoingia kwenye damu baada ya mtu kumeza dawa ni 100% na kinaonekana ndani ya masaa kumi baada ya mtu kutumia dawa.


Mwingiliano wa Treprostinil na chakula.


Dawa hii inaweza kutumika mtu akiwa amepata chakula au akiwa hajapata chakula.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Treprostinil


Wagonjwa wenye mzio wa Treprostinil ni;


Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya prostacyclin analogs.


Utoaji taka wa Treprostinil mwilini


Asilimia sabini na tisa (79%) ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia kumi na tatu (13%) hutolewa kwa njia ya haja kubwa.



Matumizi ya Treprostinil kwa mama mjamzito


Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito na mtoto aliye tumboni hivyo taadhari inatakiwa kuchukuliwa wakati mama anatumia dawa hii.


Matumizi ya Treprostinil mama anayenyonyesha


Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo kimoja wapo kati ya mtoto kunyonya na mama kutumia dawa inatakiwa viangaliwe kulingana na uhitaji .


Dawa zenye muingiliano na Treprostinil



Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Treprostinil ni Lofexidine


Dawa zinazoweza kutumika na Treprostinil chini ya uangalizi

  • Aldesleukin

  • Amifostine

  • Candesartan

  • Cannabidiol

  • Carbidopa

  • Dabigatran

  • Dichlorphenamide

  • Eluxadoline

  • Epoprostenol

  • Eprosartan

  • Fenoldopam

  • Fish oil triglycerides

  • Green tea

  • Hydralazine

  • Ibrutinib

  • Iloprost

  • Irbesartan

  • Levodopa

  • Losartan

  • Maraviroc

  • Mifepristone

  • Minoxidil

  • Olmesartan

  • Sacubitril/valsartan

  • Stiripentol

  • Tecovirimat

  • Telmisartan

  • Teriflunomide

  • Valsartan

  • Xipamide


Dawa zenye mwingiliano mdogo na Treprostinil;

  • Acebutolol

  • Amlodipine

  • Atenolol

  • Benazepril

  • Bendroflumethiazide

  • Betaxolol

  • Bisoprolol

  • Bosentan

  • Captoprii

  • Chlorothiazide

  • Chlorthalidone

  • Eplerenone

  • Epoprostenol

  • Furosemide

  • Guanfacine

  • Hydralazine

  • Hydrochlorothiazide

  • Iloprost

  • Imidapril

  • Indapamide

  • Isradipine

  • Ketanserin

  • Methyclothiazide

  • Metolazone

  • Moxonidine

  • Nadolol

  • Nifedipine

  • Nisoldipine

  • Penbutolol

  • Perindopril

  • Phenoxybenzamine

  • Phentolamine

  • Pindolol

  • Prazosin

  • Propranolol

  • Quinapril

  • Ramipril

  • Reishi

  • Shepherd's purse

  • Silodosin

  • Sotalol

  • Spironolactone

  • Terazosin

  • Timolol

  • Tizanidine

  • Torsemide

  • Trandolapril

  • Triamterene

  • Verapamil


Maudhi madogo ya Treprostinil


  • Maumivu ya tumbo

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya kichwa

  • Taya kuuma

  • Vipele

  • Maumivu ya misuli

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya mgongo

  • Vasodilation

  • Magonjwa ya ngozi

  • Cellulitis

  • Shinikizo la damu kuwa chini

  • Mapigo ya moyo kuwa juu

  • Kizunguzungu

  • Mwili kuvimba

  • Misuli kukaza

  • Maumivu ya mifupa

  • Mwili kuchoka


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Treprostinil

Imeboreshwa,

29 Oktoba 2021, 13:55:50

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page