Mwandishi:
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
Zoledronic Acid ni dawa ya kizazi cha tatu cha bisphosphonate yenye nitrogen inayofanana na to ibandronic acid, minodronic acid, and risedronic acid, inatotumika kukinga na kutibu udhaifu wa mifupa kutokana na kuzidi kwakiwango cha kalisuam kutokana na saratani na ugonjwa wa paget.
Majina mengine ya Zoledronic Acid
Majina mengine ya Zoledronic Acid ni;
Reclast
Zometa
Dawa zilizo kundi moja na Zoledronic Acid
Alendronate
Ibandronate
Etidronate
Pamidronate
Tiludronate
Fomu na uzito wa Zoledronic Acid
Dawa hii ipo katika fomu ya kimiminika kwa ajiri ya sindano chenye uzito wa;
4mg/5ml
5mg/100ml
Zoledronic Acid hutibu nini?
Hutumika kutibu kuzidi kwa kalisiamu damu kutokana na saratani
Hutumika kutibu mifupa dhaifu kwa wanawake na wanaume
Hutumika kutibu ugonjwa wa Paget
Hutumika kutibu udhaifu wa mifupa ulioamshwana homon glucocorticoid
Namna Zoledronic Acid inavyoweza kufanya kazi
Mara baada ya kuingia kwenye damu zolendronic acid hujishikiza kwenye hydroxyapatite ya mifupa. Ufyozwaji kalisiamu kwenye mifupa hutengeneza mazingira ya utindikali katika mifupa na kupelekea kuachiwa kwa zolendronic acid kutoka kwenye mifupa. Zolendronic acid hufyozwa na chembe osteoclasts kisha kuachiwa kwenye saitosol ya osteoclasts inayofanya kazi ya kufyonza mifupa. Kuzuiwa ufanyaji kazi wa osteoclasts husababisha kupungua kwa ufyozwaji wa kalisiiamu ndani ya mifupa na hivyo kufanya mifupa iwe imara kutokana na kutopoteza madini hayo.
Ufozwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ikiingia kwenye mishipa.
Mwingiliano wa Zoledronic Acid na chakula.
Dawa hii inatakiwa kutumika mtu akiwa hajala kwani chakula kinapunguza ufozwaji wa dawa.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Zoledronic Acid
Wagonjwa wenye mzio wa Zoledronic Acid.
Wagonjwa ambao calcium ipo chini (Hypocalcemia).
Utoaji taka wa Zoledronic Acid mwilini
Asilimie thelathini na tisa (39%) ya Dawa hii hutolewa njee kwa njia ya mkojo ndani ya masaa 24 na chini ya asilimia tatu (3%) hutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Matumizi ya Zoledronic Acid kwa mama mjamzito
Dawa hii hairuhusiwi kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa. Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliye tumboni hivyo hairuhusiwi kwa mama mjamzito.
Matumizi ya Zoledronic Acid mama anayenyonyesha
Dawa hii hairuhusiwi kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa.
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo hairuhusiwi kutumiwa na mama anayenyonysha.
Dawa zenye muingiliano na Zoledronic Acid
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Zoledronic Acid;
Tafiti zinaonesha kuwa hakuna dawa yenye mwingiliano mkali na Zoledronic Acid.
Dawa zinazoweza kutumika na Zoledronic Acid chini ya uangalizi;
Aluminum hydroxide
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Dichlorphenamide
Peramivir
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Sodium sulfate/?magnesium sulfate/potassium chloride
Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate
Voclosporin
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Zoledronic Acid;
Amikacin
Aspirin
Aspirin rectal
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Bumetanide
Entecavir
Ethacrynic acid
Foscarnet
Furosemide
Gentamicin
Indomethacin
Neomycin po
Paromomycin
Streptomycin
Teriparatide
Tobramycin
Torsemide
Maudhi ya Zoledronic Acid
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya mifupa
Shinikizo la damu kuwa chini
Vipele
Kichefuchefu
Haja kubwa kuwa ngumu
Kuharisha
Homa
Kutapika
Kukosa hamu ya kula
Kukosa usingizi
Kizunguzungu
Kupata woga
Madini ya magnesium kuwa chini
Mwili kuchoka
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi yako kwa wakati sahihi wasiliana na daktari wako akufahamishe muda sahihi wa kutumia dozi inayofuata.
13 Juni 2023 19:18:46
Dawa Zoledronic Acid
Imeboreshwa,
26 Septemba 2021 18:39:28
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.
Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.
Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.
Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537.
DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.
Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.
Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.
Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277.
Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29.
Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.
Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.