top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD

Dawa ya gono

31 Mei 2022 12:14:48
Image-empty-state.png

Muhimu: Soma makala hii mpaka mwisho, Kutokwa na usaha kwenye uume haimaanishi ndo gono bali ni dalili ya magonjwa ya zinaa ambayo hutibiwa kwa pamoja. Usitumie dawa pasipo ushuri wa daktari wako.


Gono au kwa jina la tiba gonorrhea hutibiwa kwa dawa jamii ya antibayotiki zilizo na nguvu ya kuua bakteria anayesababisha gono anayefahamika kwa jina la Neisseria gonorrhoeae. Ingawa dawa za kutibu gono huondoa maambukizi, dawa hizo hazina uwezo wa kuondoa madhara yaliyokwisha kusababishwa na bakteria huyu. Kupata matibabu ya gono mapema kutazuia kupata madhara yanayoweza kujitokeza.


Mgonjwa mwenye gono hutibiwa kama mgonjwa mwenye magonjwa ya zinaa, matibabu yake huhusisha dawa za kutibu vimelea vyote vinavyosababisha magonjwa ya zinaa.

Zifuatazo ni miongoni mwa dawa zinazotumiwa na wataalamu wa afya kutibu maambukizi ya Neisseria gonorrhoeae bakteria mmojawapo anayeweza kusababisha gono au kwa jina jingine kisonono;

  • Ceftriaxone

  • Azithromycin

  • Cefixime

  • Cefotaxime

  • Ceftizome

  • Erythromycin

  • Gemifloxacin

  • Gentamicin

Ili kufahamu kwa usahihi ni dawa, dozi na kwa muda gani utumie dawa ili kutibu maambukizi ya Neisseria gonorrhoeae, unashauriwa kuwasiliana na daktari wako.

Uzoefu kutoka kwa wagonjwa na madaktari wa ULY CLINIC kuhusu gono

Kati ya wagonjwa 100 wanaotafuta matibabu ya gono wagonwa 80 huwa wameshaenda famasi na kununua dawa aina ya azuma na kuitumia. Mambo ya msingi ambayo yamegundulika ni kwamba wagonjwa hao wanapopata usaha sehemu za siri hudhania kisababishi pekee ni gono na hivyo kudhani kwamba wakitumia dawa mojawapo zilizoorodheshwa hapa watapata suluhisho ambapo si sahihi. Wagonjwa hao wanapogundulika kuwa wameshatumia dawa katika kundi hili, hupewa dawa aina nyingine kwa kuwa wanakuwa wameshaharibu dozi.


Kuna mambo mbalimbali yanayochangia hali hii ambayo:

Kushindwa kutafuta na kupata taarfa sahihi- wengi wamekuwa wakipata taarifa kutoka kwa marafiki, na watu wengine waliowaita wataalamu wa afya waliowapa ushauri wa matumizi ya dawa kutibu dalili


Kutokuona umuhimu wa kuongea na daktari- wengi hawakuwa tayari kuongea hali zao na daktari ili aweze kufahamu kuhusu mnyororo wa maambukizi kwa watu wote waliohusika katika ngono ili kuhakikisha kuwa mnyororo wa maambukizi unavunjika. Hili lisipofanyika kujirudia kwa maambukizi huwa mara moja


Kutokuwa na fedha- wagonjwa wengi pia wamekuwa na changamoto ya kipato kiasi cha kutafuta urahisi wa kutumia dawa pasipo ushauri na pasipo kufahamu kuwa kutumia dozi kamili na kwa usahihi ndio njia pekee ya matibabu ya magonjwa ya zinaa.


Mambo ya kumbuka:

  • Usitumie dawa yoyote pasipo ushauri wa daktari, ULY CLINIC haitahusi na madhara yoyote yatakayojitokeza endapo umetumia dawa pasipo kushauriwa na daktari wako

  • Dawa zilizoorodheshwa hapo juu hutumika kwa kuandikiwa na daktari tu

  • Endapo una mpenzi ambaye umeshiriki naye ngono kipindi cha siku 60 zilizopita, anatakiwa kutibiwa pia kuvunja mnyororo wa maambukizi

  • Endapo una mpenzi, mpenzi wako pia anatakiwa tibiwa na wale wote unaoshiriki nao ngono pia wanapaswa kutibiwa. Usipofanya hivyo na ukashiriki nao, utapata maambukizi tena

  • Matumizi ya dawa pasipo kuandikiwa na daktari hupelekea usugu wa bakteria dhidi ya dawa hiyo

  • Vimelea vikitengeneza usugu kwenye dawa, dawa hiyo haitafaa kamwe kwenye mwili wako kwa matibabu

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
13 Julai 2023 20:07:47
1. Gonococcal Infections in Adolescents and Adults. https://www.cdc.gov/std/tg2015/gonorrhea.htm. Imechukuliwa 10.05.2022

2. Gonorrhea Treatment and Care. https://www.cdc.gov/std/gonorrhea/treatment.htm. Imechukuliwa 10.05.2022

3. Overview Gonorrhoea. https://www.nhs.uk/conditions/gonorrhoea/. Imechukuliwa 10.05.2022

4. By Sheldon R. Morris , MD, MPH. Gonorrhea. https://www.msdmanuals.com/professional/infectious-diseases/sexually-transmitted-diseases-stds/gonorrhea#. Imechukuliwa 10.05.2022
bottom of page