Mwandishi:
Dkt. Peter A, MD
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
Dawa ya kisonono
31 Mei 2022 14:45:45
Kisonono hutibiwa kwa dawa jamii ya antibayotiki zilizo na nguvu ya kuua bakteria anayesababisha gono anayefahamika kwa jina la Neisseria gonorrhoeae. Ingawa dawa za kutibu gono huondoa maambukizi, dawa hizo hazina uwezo wa kuondoa madhara yaliyokwisha kusababishwa na bakteria huyu. Kupata matibabu ya gono mapema kutazuia kupata madhara yanayoweza kujitokeza.
Mgonjwa mwenye kisonono hutibiwa kama mgonjwa mwenye magonjwa ya zinaa, matibabu yake huhusisha dawa za kutibu vimelea vyote vinavyosababisha magonjwa ya zinaa.
​
Zifuatazo ni miongoni mwa dawa zinazotumiwa na wataalamu wa afya kutibu kisonono;
Ceftriaxone
Azithromycin
Cefixime
Cefotaxime
Ceftizome
Erythromycin
Gemifloxacin
Gentamicin
​
Ili kufahamu kwa usahihi ni dawa, dozi na kwa muda gani utumie dawa ili kutibu kisonono, unashauriwa kuwasiliana na daktari wako.
Kumbuka:
​
Usitumie dawa yoyote pasipo ushauri wa daktari, ULY CLINIC haitahusi na madhara yoyote yatakayojitokeza endapo umetumia dawa pasipo kushauriwa na daktari wako
Dawa zilizoorodheshwa hapo juu hutumika kwa kuandikiwa na daktari tu
Endapo una mpenzi ambaye umeshiriki naye ngono kipindi cha siku 60 zilizopita, anatakiwa kutibiwa pia
Endapo una mpenzi, mpenzi wako pia anatakiwa tibiwa na wale wote unaoshiriki nao ngono pia wanapaswa kutibiwa. Usipofanya hivyo na ukashiriki nao, utapata maambukizi tena
Matumizi ya dawa pasipo kuandikiwa na daktari hupelekea usugu wa bakteria dhidi ya dawa hiyo
Vimelea vikitengeneza usugu kwenye dawa, dawa hiyo haitafaa kamwe kwenye mwili wako kwa matibabu