Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
Dawa ya kiungulia
2 Juni 2022 08:02:55
Dawa ya kiungulia katika makala hii imemaanisha dawa za kutuliza maumivu yanayotokea katikati ya kifua na wakati mwingine husambaa kuelekea mgongoni.
Dawa zifuatazo hutumika katika kudhibiti dalili ya maumivu ya kiungulia kwa kuzuia uzalishaji wa tindikali tumboni, chanzo kikubwa cha dalili hii. Miongoni mwa dawa hizo ni:
Cimetidine (Tagamet)
Famotidine (Pepcid)
Nizatidine
Dexlansoprazole (Dexilant)
Esomeprazole (Nexium)
Lansoprazole (Prevacid)
Omeprazole (Prilosec and another with sodium bicarbonate, Zegerid)
Pantoprazole (Protonix)
Rabeprazole (Aciphex)
Kumbuka:
Kiungulia hweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali
Dawa hizi maranyingi hupunguza dalili na si kutibu kisababishi
Wasiliana na daktari wako kuandikiwa kiasi na dozi na pia kufanyiwa uchunguzi wa kisababishi kwako ili kupatiwa tiba sahihi.