Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya kukojoa kitandani kwa watoto
11 Juni 2021 10:12:50
Dawa zilizoruhusiwa na FDA/TMDA kuzuia tatizo la kukojoa kitandani kwa watoto ni dawa ya imipramine ambayo ni dawa ya kuzuia sonona na dawa inayofanya kazi kama homoni iitwayo desmopressin acetate.
Dawa zinazotumika kuzuia kukojoa kitandani kwa watoto;
Desmopressin Acetate (DDAVP)
Hyosyamine (Levsinex)
Imipramine
Oxybutynin (Ditropan)
Dawa desmopressin na Imipramine hufanyaje kazi?
Imipramine na desmopressin acetate hufanya kazi ya;
Kupunguza kiasi cha mkojo unaozalishwa usiku
Kubadilisha mzunguko wa kulala na kuamka
Kuongeza uwezo wa kibofu kutunza mkojo
Maelezo ya ziada kuhusu desmopressin
Desmopressin inaweza kutumika yenyewe isipokuwa endapo si fanisi lazima kuungwa na dawa za anticholinejiki. Kwa kuwa Desmopressin hupunguza uzalishaji wa mkojo usiku, ukijumlisha dawa za anticholinejiki ambazo huongeza uwezo wa kibofu kutunza mkojo, tatizo la kukojoa kitandani hudhibitiwa vema.
Hyosyamine na Oxybutynin hufanyaje kazi kuzuia kukojoa kitandani?
Dawa Hyosyamine (Levsinex) na Oxybutynin (Ditropan) ni dawa aina ya anticholinejiki ambazo hazia uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea katika matibabu ya tatizo la kujikojolea kitandani, mara nyingi hutumika pamoja na Desmopressin. Dawa za anticholinejiki hufanya kazi ya;
Kuongeza uwezo wa kibofu kutunza mkojo
Maudhi ya dawa za kuacha kukojoa kitandani
Kushuka kwa shinikizo la damu
Kuhisi mapigo ya moyo
Kukauka midomo
Kichefuchefu
Haja kubwa ngumu
Uchovu
Matatizo ya usingizi
Je dawa hizo zinaweza kuzuia watoto wote kukojoa kitandani?
Hapana!
Dawa zilizoorodheshwa hapo juu zinaonekana katika tafiti kuwa huzuia kukojoa kitandani kwa baadhi ya watoto tu. Kati ya watoto 100 waliofanyiwa tafiti, watoto 19 tu waliamka wakavu wakati wamefuatiliwa kwa siku 14 na watoto 81 waliamka wamelowa mkojo kwenye baadhi ya siku.
Nini cha ziada unatakiwa kufahamu?
Kuna njia zingine za kuanza kutumia, au kutumia pamoja na dawa ili kuongeza ufanisi zaidi w akuzuia mtoto kukojoa kitandani. Soma kwenye Makala zingine za ulyclinic kuhusu 'kukojoa kitandani' na 'Dawa ya kitandani'