Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD.
Dawa za kukausha vidonda kwenye uume
16 Desemba 2024, 18:57:46

Utangulizi
Vidonda kwenye uume ni dalili inayotokea sana kwa wanaume na hutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa au magonjwa mengine yasiyoambukiza kwa njia ya ngono, pamoja na magonjwa mengine ambayo hayaambukizi mfano saratani.
Magonjwa ya zinaa yanachangia asilimia nyingi ya vidonda kwenye uume, hivyo katika makala hii dawa zilizoanishwa ni zile zinazotumika kutibu vidonda vinavyosababishwa na magonjwa ya zinaa mfano kaswende, pangusa, herpazi n.k.
Orodha ya dawa za kutibu vidonda uumeni
Dawa zinazotumika mara kwa mara kutibu au kukausha vidonda kwenye ni kama ifuatavyo;
Benzyl Penicillin (Pen G)
Azithromycin
Erythromycin
Ciprofloxacin
Doxycycline
Acyclovir
Valacyclovir
Famciclovir
Ceftriaxone
Daktari anaweza kukuandikia dawa ya kundi moja au zaidi kutokana na kisabaishi. Unapaswa kuwasiliana na daktari ili kufahamu dawa gani inakufaa wewe kulingana na kisababishi cha vidonda vyako kwenye uume.
Tahadhari kwa msomaji
Makala hii imeandikwa kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii, hivyo usitumie maelekezo yake kufanya matibabu yako.