top of page
Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, M.D
Mhariri:
Dkt. Salome A, M.D

Dawa za kutibu kuharisha

10 Julai 2023 19:40:36
Image-empty-state.png

Kuharisha hutokana na kutofyonzwa vema kwa maji maji na virutubisho  kwenye mfumo wa chakula, hii hutokana na kutofanyika vema kwa kazi hiyo ya ufyonzaji kwenye maeneo ya utumbo mwembamba na utumbo mpana.

​

Ili mgonjwa aweze kuitwa anaharisha ni lazima awe na dalili ya kupata kinyesi cha maji mara tatu (3) au zaidi kwa siku, chini ya hapo mtu anahesabika amepata choo kilaini tu.

​

Kuharisha huweza kusababishwa na maambukizi ya bakteria , vimelea, fungasi, au virusi. ni vema kupata uchunguzi wa daktarin kabla ya kutumia dawa.

​

Dawa za kuondoa/kusimamisha dalili ya kuharisha haishauriwi sana kutumia maana ni hatari. Dawa zilizoorodheshwa hapa chini hutibu kuharisha kutokana na maambukizi ya bakteria:

 

Chanjo ya kuharisha (Rotarix) kutokana na kirusi cha rotavirusi pia hutolewa hospitali. Ikumbukwe matibabu ya kuharisha kwa Watoto na watu wazima endapo tatizo sio kubwa yanaweza kuanza kwa kumpatia mtoto maji yenye ORS (Oral rehydrating solution) maji haya huwa na madini pamoja na sukari. Matumizi ya maji haya hurejesha madini na sukari iliyopotea wakati wa kuahrisha. Endapo mtoto hatapata  maji haya basi anaweza kuishiwa nguvu na kisha kulegea na kushindwa kula.

​

Endapo mtoto au mtu mzima anapata dalili hizi ni vema usisubiri au kumtibu nyumbani mwenyewe bali onana na mtaalamu wa afya haraka Zaidi.

​

  • Mtoto mwenye umri chini ya miezi mitatu

  • Uzito chini ya kilo 8

  • Mwenye historia ya kuzaliwa njiti, anayetumia dawa muda mrefu, au mwenye kuugua ugonjwa mwingine pamoja pia

  • Homa Zaidi ya nyuzi joto za Celsius 38

  • Damu kwenye kinyesi

  • Kutapika kusikoisha

  • Kuharisha sana na kwa wingi wa kinyesi

  • Dalili za kuishiwa maji mwilini kama vile macho kuzama ndani, kupungua kwa machozi, kukauka kwa midomo(lips) na kupungua kwa mkojo

  • Kubadilika kwa ufahamu

  • Kutoacha kuharisha licha ya kutumia ORS

​

Kwa maelezo zaidi soma kuhusu mada ya kuharisha kwa watoto.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
10 Julai 2023 19:40:36
BNF 2019
bottom of page