Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, M.D
Mhariri:
Dkt. Adolf S, M.D
Dawa za vibarango
11 Julai 2023 09:51:48
Vibarango kichwani husababishwa na mambukizi ya fangas, ugonjwa huo huitwa kwa jina la tinea capitis. Matibabu ya vibarango kichwani yanaweza kufanyika kwa kutumia dawa za kupaka au kumeza. Dawa za kumeza zinaweza kutumia kwa maambukizi sugu ya kujirudia rudia au endapo dawa ya kupaka si bora kutumia. Dawa za kupaka ni salama endapo mgonjwa ana Matatizo ya figo au Ini.
Dawa za kutibu fangasi huwa zinaondolewa mwilini kwa njia ya Ini na figo hivyo ni vema kuzingatia hali ya mwili wako endapo una Matatizo ya figo au Ini kwa sababu zinaweza kupelekea kuharibu ogani hizi muhimu mwilini na wakati mwingine kusababisha kifo.
Soma zaidi kuhusu vibarango kwa kubonyeza hapa.
Dawa za kutibu vibarango ni pamoja na;
Itraconazole- kwa Watoto
Ketaconazole
Majina mengine
Dawa za kutibu vibarango hufahamika pia kama;
Dawa za kutibu mashiringi kichwani
Dawa ya kutibu vibarango kichwani