top of page

Ugonjwa na dawa

Kurasa hii utajifunza kuhusu dawa na ugonjwa unaotibiwa na dawa hiyo. Wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyotee ile ili kuepuka madhara na usugu wa dawa mwilini mwako. Kumbuka siku zote kuwa dawa ni sumu kwenye mwili wako endapo haitatumika bila ushauri wa daktari

Dawa ya kutibu ugonjwa wa ngozi

Dawa ya kutibu ugonjwa wa ngozi

Kuna zaidi ya magonjwa elfu 3 ya ngozi yanayofahamika duniani, dawa za kutibu ya magonjwa ya ngozi hutegemea aina ya ugonjwa. Katika Makala hii imeorodhesha magonjwa mengi ya ngozi yanayotokea sana.

Dawa za kuyeyusha damu

Dawa za kuyeyusha damu

Dawa za kuyeyusha damu hujumuisha dawa za kufanya damu iwe nyepesi, kuyeyusha bonge la damu lililoganda au zile za kuzuia chembe sahani za damu kukusanyika ili kutengeneza bonge la damu.

Chanjo ya  kuzuia maambukizi ya HPV

Chanjo ya kuzuia maambukizi ya HPV

Virusi vya HPV wapo aina nyingi sana duniani na wengi wanaweza kusababisha magonjwa kwa binadamu saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya koo na dutu sehemu mbalimbali za mwili.

Kupata chango ya virusi vya HPV haswa kwa wanawake ni njia mojawapo ya kupunguza kupata saratani ya shingo ya kizazi.

Dawa za kutibu saratani ya shingo ya kizazi

Dawa za kutibu saratani ya shingo ya kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi imeonekana katika tafiti kusababishwa na virusi vya human papilloma (HPV) aina ya 16 na 18. Kirusi huyu huambukizwa kwa njia ya kujamiana.

Dawa za kutibu dutu ya sehemu za siri (Genital warts)

Dawa za kutibu dutu ya sehemu za siri (Genital warts)

Chunjua au dutu inafahamika pia kwenye tovuti hii kama 'maoteo sehemu za siri' ni aina mojawapo ya ugonjwa wa zinaa . Nusu ya wanaojihusisha na ngono mara kwa mara haswa isiyo salama hupata maambukizi haya kwenye muda fulani katika maisha yao na wanawake wanaathiriwa sana na haya kuliko wanaume.

bottom of page