top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

 

Dawa za kutibu chango la tumbo(antspasmodic)

Dawa za kutibu chango la tubo kwa jina la kitiba hapa ulyclinic imetumika kumaanisha dawa zinazoitwa antspasmodic. Baadhi ya dawa kundi la anticholinergic huchukuliwa kama dawa moja wapo za Antispasmodic kwa sababu hufanya kazi moja ya kutuliza misuli ya tumbo isijongee na hivyo kuondoa maumivu au chango la tumbo.

 

Dawa hizi hutumika kutibu maumivu ya tumbo ya kunyonga kutokana na kujongea kwa misuli laini ya tumbo. Matumizi ya dawa hizi yanaweza kuleta dalili ya kutopata choo au choo kigumu pamoja na maudhi mengine madogo.Orodha iliyoandikwa hapa chini inajumuisha dawa kundi la anticholinergic  na antspasmodic, wasiliana na daktari kabla ya kutumia dawa yoyote ile ili kuepuka madhara.

Dawajamii ya antispasmodic

 • Mebeverine

 • Papaverine

 • Oxybutynin

 • Trihexyphenidyl

Dawa za anticholinergic zinazotumika kutibu maumivu ya tumbo kutokana na kujongea kwa misuli laini ya tumbo

 • Dicyclomine (Bentyl)

 • Dyoscyamine (Levsin) 

 • Methscopolamine

 • Chlordiazepoxide / clidinium

 • Hyoscyamine

 • Scopolamine

 • Methscopolamine

 • Atropine

 • Mepenzolate

 • Glycopyrrolate

Kumbuka:

 • Dawa zilizoorodheshwa hapo juu hutumika kwa kuandikiwa na daktari tu

 • Matumizi ya dawa pasipo kuandikiwa na daktari hupelekea usugu wa tatizo kwenye dawa

 • Dawa zilizoandikwa hapa huondoa maumivu ya tumbo yanayosababishwa na chango au kujongea kwa misuli ya tumbo. Maumivu yanayosababishwa na matatizo mengine hayawezi tibiwa na dawa hizi. Pata uchunguzi wa daktari wako kupata dawa sahihi na kwa tatizo ashihi lililotambuliwa

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na Tiba kwa kubonyeza ‘Pata tiba’ au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

Imeboresha 05.03.2021

Rejea za mada hii;

 1.  Anticholinergics/antispasmodics. What are Anticholinergics/antispasmodics?https://www.drugs.com/drug-class/anticholinergics-antispasmodics.html Imechukuliwa 05.03.2021

 2. What are anticholinergic and antispasmodic drugs? How do they work (mechanism of action)?https://www.medicinenet.com/anticholinergics-antispasmodics-oral/article.htm. Imechukuliwa 05.03.2021

 3. Mebeverine for intestinal spasms. https://www.medicinesforchildren.org.uk/mebeverine-intestinal-spasms#. Imechukuliwa 05.03.2021

 4. Mebeverinehttps://www.nhs.uk/medicines/mebeverine/.  Imechukuliwa 05.03.2021

 5. Mebeverine. https://www.pediatriconcall.com/drugs/mebeverine/735. Imechukuliwa 05.03.2021

bottom of page