top of page

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

 

 

Dawa za Kutibu Vibarango Kichwani

​

Vibarango kichwani husababishwa na mambukizi ya fungus, ugonjwa huo huitwa kwa jina la tinea capitis. Matibabu ya vibarango kichwani yanaweza kufanyika kwa kutumia dawa za kupaka au kumeza. Dawa za kumeza zinaweza kutumia kwa maambukizi sugu ya kujirudia rudia au endapo dawa ya kupaka si bora kutumia. Dawa za kupaka ni salama endapo mgonjwa ana Matatizo ya figo au Ini

​

Dawa za kutibu fungasi huwa  zinaondolewa mwilini kwa njia ya Ini na figo hivyo ni vema kuzingatia hali ya mwili wako endapo una Matatizo ya figo au Ini kwa sababu zinaweza kupelekea kuharibu ogani hizi muhimu mwilini na wakati mwingine kusababisha kifo.

​

Dawa za kutibu vibarango ni pamoja na;

  • Griseofulvin

  • Itraconazole- kwa Watoto

  • Ketaconazole

  • Fluconazole

  • Terbinafine

bottom of page