top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Dawa za kutibu malaria

​

Dawa za kutibu malaria zipo za aina tofauti kulingana na namna zinavyofanya kazi, makala hii imeorodheshwa dawa zote zinazotibu malaria. Unaweza kubonyezapia dawa ili kusoma zaidi kuhusu matumizi na maudhi.

 

1. ALU- arthmether Lumefantrine

​

Hutibu malaria ya akyute na isiyo na maudhi

​

2. Chloroquine

 

Hutumika kama kinga ya malaria kwenye maeneo ambayo malaria ipo kwa wingi zaidi na maeneo tu ambapo ugonjwa hauna usugu na dawa hiyo. Katika maeneo ambayo vimelea vya malaria vinausugu kwenye chloroquine,  dawa hii hutumika pamoja na dawa  ya proguanil hydrochloride, hata hivo ufanisi huwa si mkubwa kukinga malaria endapo vimelea vimekuwa sugu.

 

3. Mefloquine

 

Hutumika kama kinga ya malaria kwenye maeneo ambayo vmelea vya malaria ni sugu dhidi ya dawa ya chloroquine. Dawa hii kwa sasa haitumiki kweye matibabu ya malaria kwa sababu ya usugu wa vimelea vya malaria dhidi ya dawa hii

 

4. Mchanganyiko wa piperaquine na artenimol

​

Mchanganyiko huu haishauriwai kutumika kama dawa daraja la kwanza kutibu akyuti malaria isiyo na maudhi. Dawa hiihata hivyo huwa na nusu maisha marefu kwenye damu

 

5. Primaquine

​

Hutumika kuondoa vimelea vya malaria vilivyoingia kwenye ini baada ya kutibiwa na dawa ua chloroquine. Vimelea hivyo ni vile vya P.vivax na P.ovale

​

6. Proguanil

​

Hutumika maranyingi pamoja na chloroquine lakini wakati mwingine hutumika yenyewe kama kinga ya malaria. Dawa hii haishauriwi kutumika kaa yenyewe. Malarone ambayo ni Mchanganyiko wa dawa proguanil na atovaquone  hutumika kutibu malaria isiyo na maudhi. Malarone hutumika kama kinga ya malaria inayosababishwa na kimelea cha Plasmodium falciparum endapo kunausugu wa dawa ya chloroquine, pia huweza kutumika kama mbadala wa mefloquine na doxycycline.

 

7. Pyrimethamine

​

Dawa hiihaipaswi kutumika yenyewe, hutumika pamoja na sulfadoxine kutibu malaria. Mchanganyiko wa primethamine na sulfadozine haushauriwi kutumika kama kinga ya malaria, hata hivyo hutumika kwenye matibabu ya malaria pamoja au baada  ya kutumia quinine

 

8. Quinine

​

Si dawa nzuri kama kinga ya malaria. Dawa hii hutumika kutibu malaria inayosababishwa na kimelea cha plasmodium falciparum au endapo kimelea sababishi hakifahamiki au endapo maambukizi yanasababishwa na kimelea zaidi ya mmoja.

​

9. Tetracycline

​

Katika kundi hili la dawa,dawa ya doxycycline hutumika kwa watu wazima pamoja na watoto walio zaidi ya umri wa miaka 12kama kinga ya malaria kwenye maeneo ambayo kuna usugu wa vimelea dhidi ya dawaa mefloquine na chloroquine. Dawa hii pia hutumika kama mbadala wa mefloquine na malarone

 

Dawa za kukinga kupata malaria

​

Dawa za kukinga mtu kupata malaria hushauriwa kutumika kwa watu ambao wanaishi kwenye maeneo ambapo hakuna malaria au kuna maambukizi ya chini sana. Uchaguzi wa dawa unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo;

​

  • Uwe kwenye kihatarishi ya kupata malaria

  • Usugu wa vimelea kwenye dawa

  • Ubora wa dawa kwenye  malaria hiyo

  • Maudhi ya dawa

  • Vitu vingine kama umri, ujauzito, hali ya figo na ini na uwezo wa kuzingatia dozi kinga

​

Dawa zinazoweza kutumika ni kama zilizoelezewa hapo juu

​

Dawa zingine pia hutumika kuzuia mtu asing’atwe na mbu, ubora wa dawa hizi bado haufahamiki

​

Matumizi ya nguo ndefu na neti zilizotiwa dawa ya DEET pia ni muhimu katika kujikinga na malaria

 

ULY Clini inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa maelezo zaidi na Tiba kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule wa kiafya

 

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii

​

Imeboreshwa, 27.06.2020

​

Rejea za mada hii;

​

  1. BNF 76 toleo la september-march 2018-2019

  2. Antimalaria.NHIS. https://www.nhs.uk/conditions/malaria/treatment/.Imechukuliwa 27.06.2020

  3. CDC. traveler malaria treatment. https://www.cdc.gov/malaria/travelers/drugs.html. Imechukuliwa 27.06.2020

bottom of page