Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
12 Mei 2020 17:54:04
Amiloride
Amiloride ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Potasiamu sparing diuretic. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Midamor.
Rangi ya dawa
Rangi ya dawa ni nyeupe na njano, mgonjwa ashauriwe kunywa dawa hii kama kila siku na kwa kiwango cha dozi alichopewa.
Fomu na uzito wa dawa
Amiloride hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;
5 mg
10 mg
Namna dawa inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuzuia utendaji kazi wa homoni ya Aldosterone ambayo hufanya kazi ya kuthibiti kiasi cha sodiamu na maji kwenye damu. Kuzuiwa kwa utendaji kazi wa homoni hii husababisha kupotea kwa maji na chumvi mwilini na hivyo kupunguza kiwango cha damu katika mishipa ya damu na hatimaye shinikizo la damu hupungua. Dawa hii pia huzuia kupotea kwa kiwango cha potasiamu kwenye damu, hii ndo maana kundi la dawa limeitwa kwa jina la Potasiamu sparing diuretics
Dawa zingine zilizo kundi moja
Triamterene
Spironolactone
Eplerenone
Kazi ya dawa
Hutumika kwa wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu
Hutumika kwenye matibabu ya shinikizo la damu kwa wagonjwa wa moyo ulioferi
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na dawa hii
Cyclosporine
Drospirenone
Eplerenone
Lofexidine
Potassium acid phosphate
Potassium Chloride
Spironolactone
Tafenoquine
Triamterene
Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa hii
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au zingine katika kundi lake
Wagonjwa wenye Haipakalemia
Haipaswi kutolewa pamoja na dawa yeyote ya Potasiamu bSparing Diuretic
Wagonjwa wenye figo iliyoferi na magonjwa sugu ya ini
Tahadhari ya dawa hii
Dawa hii huweza kupelekea kupoteza madini mwilini ikiwa Pamoja na madni ya sodiamu.
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye matatizo ya ini na figo
Matumizi kwa mama mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito endapo kuna uhitaji. Tafiti zilizofanyika kwa wanyama zinaonyesha kuwa Wanyama hao hawakupata madhara yoyote katika ujauzito wao.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu huingia kwenye maziwa ya mama na hivyo mtoto ataipata kwa kunywa maziwa ya mama.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa
Haipakalemia
Kukosa hamu ya kula
Kichwa kuuma
Kichefuchefu
Maumivu ya tumbo
Kukohoa
Kukohoa
Kizunguzungu
Kuchoka
Kuishiwa pumzi
Nusu maisha ya dawa
Amiloride mara nyingi huanza kufanya kazi ndani ya masaa 2 baada ya kozi ya kunywa. Madhara ya kitiba ya dawa hufika kileleni ndani ya masaa 6 hadi 9 na hudumu kwa masaa 24. Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 3 hadi 4 na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 6 hadi 9.
Utoaji dawa mwilini
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia 50 na njia ya kinyesi kwa asilimia 40 ndani ya masaa 72.
Je kama umesahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau kunywa dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na ikiwa muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-