top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

28 Mei 2020 19:01:39

Azithromycin

Azithromycin

Azithromycin yenye jina jingine la Zithromax, ni dawa jamii ya antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria iliyo kwenye kundi la macrolide. Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge, tembe na kimiminika kwa ajili ya kunywa au kimininika kwa ajili ya kutumika kwa kuchoma sindano.

Fomu ya dawa


Hupatikana kwenye fomu ya Tembe yenye uzito wa miligramu 250 au 500

Ufyonzwaji wa Azithromycin


 • Mara baada ya kunywa kidonge chenye miligramu 250, asilimia 38 tu ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye mzunguko wa damu.

 • Utoaji wa mabaki ya Azithromycin

 • Nusu maisha ya dawa ni masaa 68, dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na kinyesi

Mwingiliano wa Azithromycin na dawa zingine


 • Kutumia dawa hii pamoja na Efavirenz au fluconazole huleta mwingiliano wa wastani. Dawa ya nelfinavir huongeza kiwango cha dawa hii kwenye damu.

 • Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Azithromycin


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja nadawa zifuatazo;


 • Warfarin

 • Venetoclax

 • Vemurafenib

 • Vandetanib

 • Umeclidinium bromide/vilanterol

 • Toremifene

 • Topotecan

 • Saquinavir

 • Riociguat

 • Rimegepant

 • Protamine

 • Pomalidomide

 • Pimozide

 • Phenindione

 • Panobinostat

 • Ondansetron

 • Macimorelin

 • Lefamulin

 • Inotuzumab

 • Hydroxychloroquine sulfate

 • Heparin

 • Glasdegib

 • Fondaparinux

 • Enoxaparin

 • Dronedarone

 • Digoxin

 • Dalteparin

 • Colchicine

 • Cobicistat

 • Cisapride

 • Cholera vaccine

 • Chanjo hai ya bcg

 • Bivalirudin

 • Bemiparin

 • Arsenic trioxide

 • Argatroban

 • Antithrombin III

 • Antithrombin alfa

Namna Azithromycin inavyofanya kazi


 • Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia kutengenezwa kwa vijenzi muhimu vya bakteria. Hufanya hivyo kwa kupinga utendaji kazi wa vinasaba vya bakteria.

 • Bakteria wanashambuliwa na azithromycin

 • Dawa hii hutumika kwenye matibabu yaliyoosababishwa na bakteria wafuatao’


Bakteria Gram-positive


 • Staphylococcus aureus

 • Streptococcus agalactiae

 • Streptococcus pneumoniae

 • Streptococcus pyogenes

 • Beta-hemolytic streptococci (Groups C, F, G)

 • Viridans group streptococci


Bakteria gram-negative


 • Haemophilus ducreyi

 • Haemophilus influenzae

 • Moraxella catarrhalis

 • Neisseria gonorrhoeae

 • Bordetella pertussis


Bakteria wa anaerobiki


 • Peptostreptococcus species

 • Prevotella bivia

Bakteria wengine


 • Chlamydophila pneumoniae

 • Chlamydia trachomatis

 • Mycoplasma pneumonia

 • Ureaplasma urealyticum

 • Legionella pneumophila

Magonjwa yanayotibiwa na Azithromycin


 • Maambukizi ya muda mfupi ya bakteria kwa wagonjwa wa COPD

 • Maambukizi ya muda mfupi ya sinusaitizi iliyosababishwa na bakteria

 • Nimonia ya jamii

 • Pharynjaitis/tonsilaitizi

 • Maambukizi ya ngozi yasiyo sugu

 • Urethritizi and servisaitizi

 • Vidonda sehemu za siri kutokana na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende


Tafiti mpya za mwaka 2020 zinaonyesha kuwa Azithromycin inaweza kuzuia uzalianaji wa virusi vinavyosababisha COVID-19. Soma zaidi katika makala ndani ya tovuti hii inayohusu dawa za kutibu COVID-19 kupata maelezo zaidi kuhusu namna dawa hii inavyofanya kazi kwenye matibabu ya COVID-19


Wakati gani usitumie dawa ya Azithromycin


Una mzio na dawa hii au dawa zingine jamii ya macrolide au ketolide pia kama uliwahi pata manjano ya cholestatiki


Tahadhari


 • Husababisha mzio

 • Huongeza muda wa QT kwenye moyo

 • Huwa sumu kwenye ini- endapo dalili za hepataitiz zinatokea acha mara moja kuendelea na dozi ya dawa hii. Dalili ni manjano, kuferi kwa ini na nekrosisi kwenye ini.

 • Tumia kwenye matibabu ya nimonia iliyosababishwa na bakteria aina ya Chlamydia pneumoniae, Haemophilus influenzae, Mycoplasma pneumoniae au Streptococcus pneumonia

 • Hupelekea kuharisha kutokana na maambukizi ya clostridium deficile


Taarifa muhimu kwa mgonjwa kuhusu Azithromycin


Dawa hii inaweza kutumiwa pamoja au pasipo chakula. Unapotumia dawa hii hakikisha hautumii sambamba na dawa za kupunguza uzalishaji tindikali jamii ya aluminium na magneziamu.


Matumizi ya Azithromycin kipindi cha ujauzito na kundi lake kipindi cha ujauzito


Dawa hii ipo kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Matumizi wakati wa ujauzito


Hakuna tafiti za kutosha kuhusu madhara wakati wa ujauzito kwa kichanga. Itumike kwa tahadhari endapo inahitajika.


Kwa mama anayenyonyesha


Haifahamiki kama dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama au la. Kwa sababu dawa nyingi huingia kwenye maziwa ya mama, tahadhari inatakiwa kuchukuliwa endapo dawa hii itatumika kwa mama anayenyonyesha


Maudhi ya Azithromycin


 • Kuhisi mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo

 • Maumivu ya kifua

 • Tumbo kujaa gesi\kujamba

 • Kutapika

 • Choo cheusi

 • Manjano ya kolestatiki

 • Miwasho ukeni

 • Nefraitizi

 • Maumivu ya kichwa, kizunguzungu

 • Kuhisi vitu vinazunguka

 • Huzuniko

 • Uchovu

 • Harara kwenye ngozi

 • Kuongezeka hisia za macho kwenye mwanga na

 • Angioidima

Ufanye nini endapo umesahau dozi yako ya Azithromycin?


Endapo umesahau kunywa dozi yako, kunywa mra pale utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi umekaribia sana, acha na kunywa dozi inayofuata. Usinywe dozi mbili kwa wakati mmoja.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

bottom of page