Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
18 Aprili 2020 18:48:56
Buformin
Ni dawa ya kumeza inayotumika katika matibabu ya ugonjwa wa kisukari, dawa hii ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa Biguanide.
Buformin kwa sasa imeondolewa sokoni kutokana na madhara yake ya kusabababisha laktiki asidosisi- hii ni hali ambayo uzalishaji wa laktiki asidi huwa mkubwa pale hewa ya oksijeni inapokuwa ndogo kweney misuli.
Dawa zilizo kundi moja na Buformin
Proguanil
Phenformin
Chlorhexidine
Metformin
Chlorproguanil
Cycloguanil
Jinsi Buformin inavyofanya kazi
Hufanya kazi ya kupunguza kiasi cha sukari kinachotolewa na Ini kwenda kwenye damu.
Hupunguza ufyozwaji wa glukosi kwenye utumbo mdogo
Hufanya seli Beta za kongosho kuzalisha homoni ya insulin
Kazi za dawa ya Buformin
Ilikuwa ikitumika kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili ambacho mara nyingi uzalishwaji wa Insulin huwa mdogo . Lakini kwa sasa haitumiki kutokana na athari zake za kusabababisha Laktiki Asidosisi
Tahadhari ya Buformin
Utumiaji wa pombe huweza kupelekea hali mbaya ya laktiki asidosisi
Husababisha tezi ya adreno kushindwa kufanya kazi vizuri
Husababisha tezi pituitari kushindwa kufanya kazi zaidi
Huweza kuathiri ufyozwaji wa Vitamin B12
Matumizi ya Buformin Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama wajawazito na wamama wanaonyonyesha
Maudhi ya Buformin
Choo kilaini
Kuchoka
Laktiki asidosisi-ni hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha laktiki asidi inayozalishwa na misuli kutokana nakiwango kidogo ha oksijeni kwenye misuli.
Kichefuchefu
Kutapika
Kukosa hamu ya kula
Maumivu ya tumbo
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:47:57
Rejea za mada hii:-