top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

2 Mei 2020 20:48:07

Candesartan

Candesartan

Candesartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa angiotensini II Risepta bloka. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Atacand.


Rangi ya Candesartan


Rangi ya dawa hii ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza


Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa. Dozi utakayopewa itategemea hali yako ya kiafya na jinsi mwili unavyokubali matibabu


Kukusaidia kukumbuka dozi yako, tumia muda sawa wa kunywa dawa kila siku. Ni muhimu kuendelea kutumia dawa hii hata kama haujisikii kuumwa maana mara nyingi wagonjwa wa shinikizo la juu la damu huwa hawaonyeshi dalili za kuumwa.


Candesartan hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;

  • 4mg

  • 8mg

  • 16mg

  • 32 mg


Namna dawa inavyofanya kazi ili kupunguza shinikizo la damu;


Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na Candesartan hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu;


Hufanya kazi kwa kufunga risepta za Angiotensin II zinazojulikana kwa jina la AT1 Risepta. Risepta hizi hupatikana kwenye moyo,mishipa ya damu na figo. Risepta hizi zinapofungwa hupelekea kutanuka kwa mishipa ya damu hivyo kuwa na kipenyo kikubwa na matokeo yake ni kushuka kwa shinikizo la damu.


Hupinga uzalishwaji wa homoni ya Aldosterone ambayo hutumika kuthibiti kiasi cha sodium na maji. Kiasi cha sodiamu kinapothibitiwa huweza kupunguza shinikizo la damu kwa hutanua kipenyo cha mishipa ya damu na kuruhusu damu kupita bila shinikizo la juu


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la ARBs) ni;


  • Azilsartan

  • Olmesartan

  • Eprosartan

  • Irbesartan

  • Losartan

  • Telmisartan


Kazi ya dawa


Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (ARBs)


Tafiti zinaonyesha Candesartan huweza kupunguza hatari ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo, kiharusi,moyo na figo kuferi na Retinopathi.


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


  • Benazepril

  • Captopril

  • Enalapril

  • Fosinopril

  • Lisinopril

  • Lithium

  • Lofexidine

  • Moexipril

  • Perindopril

  • Potassium Phosphate IV

  • Quinapril

  • Ramipril

  • Trandolapril


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za ARBs pia haipaswi kutumika pamoja na dawa ya Aliskiren kwa wagonjwa wa kisukari


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wagonjwa wenye historia ya angioedema

  • Wagonjwa wenye Haipotension

  • Wagonjwa wenye shida ya figo

  • Wagonjwa wenye haipovolemia


Kundi la dawawakati wa ujauzito


Dawa hii ipo kwenye kundi D la usalama wa dawa wakati wa ujauzito


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Kwa mama mjamzito inapaswa kusimamishwa punde tu mama atakapokuwa na ujauzito kwa sababu dawa hii huwa na madhara kwa mtoto kama haipotension,figo kuferi na kifo.


Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama inatolewa kwenye maziwa


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;

  • Kichwa kuuma

  • Kizunguzungu

  • Haipaglycemia

  • Maumivu ya mgongo

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuharisha

  • Maumivu kwenye misuli

  • Kuchoka

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya kifua


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:48:32

Rejea za mada hii:-

1.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasawa 156

2.Goodman and Gilman’s The Pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428 Ukurasa wa 722

3.Clinical pharmacology and therapeutics Written by James M Ritter ISBN 978-0-340-90046-8 ukurasa wa 188

4.WebMd.Candesartan.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-4682/candesartan -oral/details. Imechukuliwa 1/5/2020

5.MedScape.Candesartan.https://reference.medscape.com/drug/lotensin-candesartan-342327.Imechukuliwa 1/5/2020

6.FDA. Candesartan. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2005/020838s022lbl.pdf. Imechukuliwa 1/5/2020
bottom of page