top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

4 Mei 2020 21:28:33

Cimetidine

Cimetidine

Cimetidine ni dawa ambayo inazuia kutolewa kwa histamine na hivyo kuzuia kutengezwa kwa tindikali tumboni. Hivyo dawa hii hutumika kutibu matatizo mbalimbali yanayotokana na tindikali ya tumboni.


Majina mengine


  • Tagamet

  • Eureceptor

  • Tametin

  • Dyspamet

  • Ulcedine


Fomula ya kikemikali


C10H16N6S


Jina la kisayansi (IUPAC)


1-cyano-2-methyl-3-[2-[(5-methyl-1H-imidazol-4-yl) methylsulfanyl] ethyl] guanidine


Dozi zinazo patikana


Dozi ya kuchoma kwa sindano;

Miligramu 150/mL


Dozi ya kimiminika;

Miligramu 30/5mL


Dozi ya vidonge;

  • Miligramu 200

  • Miligramu 300

  • Miligramu 400

  • Miligramu 600

  • Miligramu 800


Matumizi ya dawa ya cimetidine


Dawa hii inatumika kutibu hali zifuatazo;

  • Vidonda vya tumbo

  • Kiungulia

  • Kucheua gesi (ugonjwa wa Gastroesofajio refluksi)

  • Kutibu michubuko kwenye koo la chakula iliyo sababishwa na michubuko ya tindikali (kiungulia).

  • Husaidia kuzuia damu kuvuja kwenye njia ya juu ya mfumo wa chakula.

  • Hutumiwa wakati mgonjwa akipewa dawa ya usingii kwa dharura ili kuzuia mgonjwa asipaliwe na tindikali kutoka tumboni.

  • Kutibu hali ya kutengenezwa kwa tindikali kupita kiasi tumboni (sindromu ya Zollinger-Ellison).


Namna dawa inavyofanya kazi mwilini


Dawa hii inazuia kutengenezwa kwa tindikali tumboni hususani mara baada ya kula chakula. Kwa kuzuia kuzalisha tindikalia inasaidia kutibu kingulia na vidonda vya tumbo na shida nyingine kutokana na tindikali tumboni.


Mwili unachofanya kwa dawa hii


  • Hufyonzwa kwa asilimia 60-70 kutoka kwenye mfumo wa chakula baada ya kumezwa.

  • Huanza kufanya kazi dakika 30, baada ya kumeza.

  • Ufanyaji kazi wake hufika kilele baada ya saa 1 – 3.

  • Huweza kufanya kazi mwilini kwa saa 4- 8.

  • Dawa hii huchakatwa na mwili kwenye ini ili kufanya kazi na kuondoa sumu.

  • Nusu Maisha ya dawa hutumika mwilini baada ya saa 2.

  • Taka mwili za dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo.


Maudhi madogo madogo


  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kuharisha

  • Usingizi

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuchanganyikiwa hususani kwa wazee

  • Kizunguzungu

  • Mara chache inaweza kupunguza uwezo wa kufanya tendo kwa wanaume.

  • Pia imeripotiwa kuwa matumizi ya muda mrefu sana yanaweza kusababisha mwanaume kuota maziwa kama wanawake. Hili ni kwa 0.1% hadi 0.2%.

  • Matumizi ya dawa hii kupita mshipa yanaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi, au shinikizo la damu kushuka.


Marufuku kwa wagonjwa wafuatao


Wagonjwa wenye aleji na cimetidine.


Muingiliano na dawa nyingine


  • Dawa zifuatozo hupunguza ufyonzwaji wa cimetidine;

  • Sodium bicarbonate

  • Calcium carbonate

  • Magnesium dihydroxide

  • Magnesium carbonate

  • Magnesium trisilicate

  • Aluminium hydroxide

  • Metoclopramide


Dawa zifuatazo huongeza uwezekano wa madhara mwilini kama zikitumiwa pamoja na cimetidine;


  • Anisindione

  • Warfarin

  • Heparin

  • Phenytoin

  • Quinidine

  • Lidocaine

  • Theophylline

  • Kutumia cimetidine pamoja na morphine kunaongeza hatari ya kushindwa kupumua.

  • Cimetidine hupunguza kiwango cha digoxin kwenye damu kama zikitolewa kwa pamoja.


Muingiliano na chakula


  • Epuka kunywa pombe unapotumia cimetidine.

  • Unaweza kutumia na pamoja na chakula.

  • Punguza matumizi ya vinywaji vyenye kafein kama vile kahawa.


Kundi la dawa kipindi cha ujauzito


Dawa ya cimetidine ipo katika kundi B la usalama wa dawa wakati wa ujauzito.


Matumizi kwa wakati wa ujauzito na kunyonyesha


Dawa inaweza kutumika; Majaribio kwa wanyama yameonesha madhara na majaribio kwa binaadamu hayajafanyika. Au majaribio kwa wanyama yameonesha madhara kidogo na majaribio kwa binadamu hayajaonesha madhara.


Matumizi wakati wa kunyonyesha


Wakati wa kunyonyesha ni vyema kuepuka matumizi ya cimetidine wakati wa kunyosha na kutumia dawa salama Zaidi ili kuepuka madhara kwa mtoto anye nyonya.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.Goodman & Gilman’s The Pharmacological Basis of THERAPEUTICS twelfth edition ISBN: 978-0-07-176939-6 ukurasa wa 1313.

2.A Textbook of Clinical Pharmacology and TherapeuticS Fifth ISBN 978-0-340-90046-8 ukurasa wa 250.

3.Medscape: https://reference.medscape.com/drug/tagamet-cimetidine-341984#4. Imechukuliwa 30/04/2020.

4.Drug bank: https://www.drugbank.ca/drugs/DB00501. Imechukuliwa 30/04/2020.

5.FDA. Cimetidine. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/anda/98/75285_Cimetidine.pdf. Imechukuliwa 30/04/2020.
bottom of page