top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

24 Aprili 2020 06:11:58

Clozapine

Clozapine

Clozapine ni dawa kizazi kipya katika kundi la dawa za atipiko antisaikotiki, dawa hii hufahamika kama serotonini na dopamine inhibita kwa kuwa huzuia ufanyaji kazi wa homoni ya serotonin na dopamine kwenye mfumo wa kati wa fahamu ili kuleta madhara ambayo ndo kiini cha tiba yake. Clozapine hutumiwa katika matibabu ya ugonjwa wa skizofrenia iliyo sugu kwenye dawa tiba elekezi.


Dawa hii inapaswa kutumika lisaa limoja kabla au baada ya kula, haipaswi kutumika pamoja na chakula kwa kuwa ufyonzaji wake hupugua.


Mara baada ya kunywa dawa hii, inachukua muda wa wiki kadhaa (wiki 6 kwa mgonjwa wa skizofrenia) kabla ya dalili kuanza kupotea, unashauriwa kuendelea kutumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari wako katika kipindi hiko.


Ufyonzwaji wa dawa tumboni


Dawa hii mara unapoinywa hufyonzwa kwenye utumbo kwa asilimia 90 hadi 95 ya dawa. Ndani ya saa 1-2 dawa hufikia kilele chake kwenye damu.


Uchakatuaji wa dawa mwilini


Umetaboli inafanyika kwenye Ini na mabaki ya dawa hutolewa kwa njia ya kinyesi kwa asilimia 30 na asilimia 50 kwa njia ya mkojo.


Dawa hii hutibu


  • Kudhibiti halusinesheni

  • Kupunguza dalidali za mhemko kuhusishwa na wasiwasi

  • Kuthibiti mawazo yakujirudia ya kutaka kijidhuru ama kujiua

  • Kutibu matatizo ya usingizi

  • Kutibu ugonjwa wa kihisia


Maudhi madogo madogo ya dawa


  • Agranulosaitosisi

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Kupata kiungulia

  • Kuharisha

  • Upele katika ngozi

  • Kizunguzungu

  • Kuongezeka hamu ya chakula

  • Kuvimbiwa

  • Maumivu ya tumbo

  • Ongezeko la uzito wa mwili

  • Kutokwa na jasho jingi

  • Kuweweseka

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuanguka

  • Kusinzia

  • Udhaifu wa mwili

  • Haipagkaisemia

  • Dayabetiki ketoasidosisi


Angalizo


Tumia dawa hii kwa Umakini kwa watu

  • Wenye matatizo ya Ini

  • Wenye shinikizo la damu, matatizo sugu ya moyo

  • Wenye matatizo ya Kifafa

  • Wenye matatizo ya Figo

  • Wenye aleji na dawa hii na pamoja na aleji nyingine

  • Wenye matatizo ya kukosa fahamu

  • Wenye magonjwa ya damu mfano leukemia

  • Wenye kisukari


Usitumie dawa hii pamoja na


  • Usitumie dawa hii pamoja na dawa za kutibu shinikizo la damu la juu

  • Usitimie dawa hii pamoja na dawa jamii ya antidepressants mfano fluvoxamine

  • Usitumie dawa hii pamoja na baadhi ya antibiotiki mfano ciproflaxin

  • Usitumie dawa hii pamoja dawa za kifafa mfano carbamazepine

  • Usitumie kama unamzio na dawa hii


Kwa Wajawazito


Itumiwe endapo kuna umuhimu katika ujauzito


Kwa Wanaonyonyesha


Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha. Sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyeshwa.


Ukisahau dose Nini kifanyike


Kama umesahau kunywa dose yako, kunywa mara tu unapokumbuka, endapo muda wa dozi nyingine umefika, ruka hiyo dozi uliyosaau na kuendelea na dozi yako kwa muda uliopangiwa. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:46:38

Rejea za mada hii:-

1.Clozapine Uses, side effects, Interactions. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-5200/clozapine-oral/details. Imechukuliwa 21.4.2020

2.Pubmed- Disanto AR etal. Effect of food on the pharmacokinetics of clozapine orally disintegrating tablet 12.5 mg: a randomized, open-label, crossover study in healthy male subjects. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/19591515. Imechukuliwa 21.03.2020

3.Clozapine.https://www.drugs.com/clozapine.html. Imechukuliwa 21.4.2020

4.Clozapine. https://www.rxlist.com/consumer_clozapine_clozaril/drugs-condition.htm. Imechukuliwa 21.4.2020

5.Clozapine. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00363. Imechukuliwa 21.4.2020

6.FDA. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2010/019758s062lbl.pdf. Imechukuliwa 21.03.2020

7.Clozapine. https://www.medsafe.govt.nz/profs/datasheet/c/Clozariltab.pdf. Imechukuliwa 21.03.2020
bottom of page