Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Septemba 2021, 12:33:57

Dawa Etidronate
Etidronate ni moja kati jamii ya bisphosphonate inayotumika kutibu kukinga na kutibu magonjwa ya magonjwa ya mifupa kama ugonjwa wa paget unaosababisha mifupa kuwa dhaifu na kuvunjika.
Majina mengine ya Etidronate
Majina mengine ya Etidronate ni;
Didronel
Etidronic acid
Fomu ya dawa ya Etidronate
Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge chenye uzito wa;
200mg
400mg
Dawa zilizo kundi moja na Etidronate
Dawa zilizo kundi moja na Etidronate ni ;
Risedronate
Ibandronate
Alendronate
Pamidronate
Zoledronate
Namna Etidronate inavyoweza kufanya kazi
Dawa jamii ya Bisphosphonates kama ikiwa pamoja na Etidronate hufyonzwa na chembe na mifupa kisha kujishikiza kwenye hydroxyapatite. Kujishikiza huku husababisha kutengeneza mazingira ya utindikali na kuzalishwa kwa bisphosphonate inayosaidia chembe za osteoclast kuzuia kufyonzwa kwa kwa madini kalisiamu yaliyo kwenye mifupa.
Etidronate hutibu nini?
Hutumika kutibu ugonjwa wa paget
Hutumika kutibu Heterotopic ossification
Hutumika kukinga udhaifu wa mifupa ulioamshwa na-PTH
Hutumika kukinga mayosaitiz ossificans endelevu
Hutumika kukinga kalsinosis universalis
Ufozwaji wa Etidronate
Asilimia 1 hadi 10 ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye mzunguko wa damu kama ikitumika kwa kunywa.
Mwingiliano wa Etidronate
Dawa hii inatakiwa kutumika mtu akiwa hajala kwani chakula kinapunguza ufozwaji wa dawa. Vyakula vifuatavyo zinashauriwa kutotumika ndani ya masaa mawili kabla au baada ya kunywa dawa
Vyakula vyenye madini kalisiamu kwa wingi kama mazwa na mazao ya maziwa
Vidonge vyenye vitamin nyongezeza na madini kama kalisiamu, chuma, magnesium au aluminum.
Utoaji taka wa Etidronate mwilini
Dawa hii haibadirishwi kwenye mkojo, dawa ambayo haijafozwa hutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Etidronate
Wagonjwa wenye mzio wa Etidronate
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya bisphosphonate
Dawa zenye muingiliano na Etidronate
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Etidronate;
Hakuna orodha ya dawa yenye muingiliano mkali na Etidronate.
Dawa zinazoweza kutumika na Etidronate chini ya uangalizi;
Aluminum hydroxide
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Deferasirox
Magnesium ya nyongeza
Selenium
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Sodium sulfate/?magnesium sulfate/potassium chloride
Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate
Voclosporin
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Etidronate;
Entecavir
Foscarnet
Teriparatide
Maudhi madogo ya Etidronate;
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya mifupa, misuli na viungio vya mwili
Degedege
Homa
Madini ya calcium kupungua
Madini ya magnesium kupungua
Phospatemia kupungua
Figo kushindwa kufanya kazi vizuri
Kuchanganyikiwa
Msongo wa mawazo
Kuona vitu visivyokuwepo
Vipele
Kupoteza radha
Kupata vidonda vya tumbo
Matumizi ya Etidronate kwa mama mjamzito
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliye tumboni hivyo tahadhari inatakiwa wakati wa kutumia hii dawa.
Matumizi ya Etidronate mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo tahadhari inatakiwa ichukuliwe wakati wa kutumia dawa hii.
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi kwa wakati sahihi tumia pale utapokumbuka kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau subiri kuendelea na dozi inayofata kwa muda sahihi. Usitumie dozi mbili kufidia ile uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:56:16
Rejea za mada hii:-