Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020 05:27:17
Dawa ya Cefadroxil
Cefadroxil ni aina ya dawa iliyo kwenye daraja la kwanza la antibayotiki jamii ya Cephalosporin. Dawa hii hutumika kupambana na maambukizi mbalimbali kwenye mwili yanayosababishwa na bakteria.
Majina mengine ya Cefadroxil
Cefadroxil huwa maarufu kwa majina ya Duricef na ultracef, sandrox-500
Rangi, uzito na fomu ya Cefadroxil
Rangi ya dawa ni ya machungwa lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza Cefadroxil hupatikana katika mfumo wa tembe,maji na kidonge wenye uzito wa; Tembe
500 mg
Kimiminika cha vial
250mg/5mL
500mg/5mL
Kidonge
1 g
Namna cefadroxil inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa peptidoglacan ambayo huunda ukuta wa seli kwenye bakteria ,Kwa kufanya hivyo hupelekea kufa kwa bakteria
Dawa zilizo kundi mojana cefadroxil
Cefazolin
Cephalexin
Cephalothin
Cephapirin
Cephradine
Kazi ya cefadroxil
Hutumika kwenye matibabu ya tezi kuvimba
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye pharyngitis
Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ya mfumo wa mkojo
Utofauti wa Cefadroxil na dawa zilizo kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la cephalosporin daraja la kwanza ni:
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine.
Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni saa 1 mpaka saa 2 tangu itumike mwilini
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Cefadroxil
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Antithrombin alfa
Argatroban
Bivalirudin
Dalteparin
Enoxaparin
Fondaparinux
Heparin
Warfarin
Bazedoxifene
Dienogest
Estradiol
Ethinylestradiol
Probenecid
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cefadroxil
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za cephalosporin
Tahadhari kwa watumiaji wa Cefadroxil
Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo Matumizi ya muda mrefu huweza kupelekea fangasi kwenye mwili
Matumizi ya Cefadroxil kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito ,Tafiti za wanyama hazionyeshi hatari yeyote kwa mjamzito
Matumizi ya Cefadroxil kwa mama anayenyonyesha
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya Cefadroxil
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Homa
Ukisahau kutumia dozi ya Cefadroxil
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ? Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 17:22:43
Rejea za mada hii:-