top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

27 Oktoba 2020 05:52:54

Dawa ya Cephapirin

Dawa ya Cephapirin

Cephapirin ni aina ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la kwanza la antibayotiki jamii ya Cephalosporin. Dawa hii hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya cefapirin.


Rangi na fomu ya Cephapirin


Cephapirin hupatikana katika mfumo wa unga mweupe kwa ajili ya kuchanganya na maji kabla ya uchoma kwenye mishipa. Uzito wa unga huu huwa gramu(g) • 1g • 2g • 10g


Namna Cephapirin inavyofanya kazi


Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa peptidoglacan ambayo huunda ukuta wa seli kwenye bakteria ,Kwa kufanya hivyo hupelekea kufa kwa bakteria


Dawa zilizo kwenye kundi moja na Cephapirin


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Cephalosporin dalaja la kwanza ni ;

• Cefazolin • Cefadroxil • Cephalothin • Cephapirin • Cephradine


Kazi ya Cephapirin


Hutumika kwa ajili ya kutibu Maambukizi mbalimbali ya magonjwa yanayosababishwa na Bakteria


Usitumie Cephapirin pamoja na dawa hizi


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo • Argatroban • Bivalirudin • Dalteparin • Enoxaparin • Fondaparinux • Heparin • Warfarin • Bazedoxifene • Dienogest • Estradiol • Ethinylestradiol • Probenecid


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cephapirin


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za cephalosporin


Tahadhari ya Cephapirin


• Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo • Matumizi ya muda mrefu huweza kupelekea fangasi kwenye mwili


Matumizi ya Cephapirin kwa mama mjamzito


• Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito • Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito. Tafiti za wanyama hazionyeshi hatari yeyote kwa mjamzito


Matumizi ya Cephapirin kwa mama anayenyonyesha


Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa


Maudhi ya Cephapirin


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Maumivu ya tumbo • Kichefuchefu • Kutapika • Kuharisha • Homa


Endapo umesahau dozi ya Cephapirin


Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1.PubChem.Cephapirin.https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Cephapirin. Imechukuliwa 31/9/2020

2.DrugBank.Cephapirin.https://www.drugbank.ca/drugs/DB01139. Imechukuliwa 31/8/2020

3.PubChem.Cephapirin.https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Cephapirin-sodium. Imechukuliwa 31/9/2020

4.VetMedia.Cephapirin.https://www.bi-vetmedica.com/species/cattle/products/ToDay.html. Imechukuliwa 31/9/2020
bottom of page