Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020 05:56:41
Dawa ya Cephradine
Cephradine ni aina ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la kwanza la antibayotiki ya Cephalosporin. Dawa hii hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya Intracef na Velocef
Fomu na rangi ya Cephradine
Rangi ya dawa ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza Cephradine hupatikana katika fomu ya tembe na kidonge vyenye uzito wa milligramu zifuatazo: Tembe
• 250 mg • 500 mg • 750 mg Kidonge
• 250 mg • 500 mg
Namna Cephradine inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa peptidoglacan ambayo huunda ukuta wa seli kwenye bakteria ,Kwa kufanya hivyo hupelekea kufa kwa bakteria
Dawa zilizo kwenye kundi moja la Cephradine
• Cefazolin • Cefadroxil • Cephalothin • Cephapirin • Cephalexin
Kazi ya Cephradine
• Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye pharyngitis • Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ya mfumo wa mkojo • Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi kwenye sikio
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Cephradine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo; • Argatroban • Bivalirudin • Dalteparin • Enoxaparin • Fondaparinux • Heparin • Warfarin • Bazedoxifene • Dienogest • Estradiol • Ethinylestradiol • Probenecid
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cephradine
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za cephalosporin
Tahadhari kwa watumiaji wa Cephradine
• Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo • Matumizi ya muda mrefu huweza kupelekea fangasi kwenye mwili
Matumizi ya Cephradine kipindi cha ujauzito
• Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito • Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito ,Tafiti za wanyama hazionyeshi hatari yeyote kwa mjamzito
Mtumizi ya Cephradine kwa mama anayenyonyesha
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya dawa Cephradine
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Maumivu ya tumbo • Kichefuchefu • Kutapika • Kuharisha • Homa
Endapo umesahau dozi ya Cephradine
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-