Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Agosti 2020 16:54:26
Dawa ya Cicloprox
Ciclopirox ni dawa ya antifangasi ya kutengenezwa kiwandani inayotumika katika matibabu ya maradhi yanayosababishwa na fangasi wanadhuriwa na dawa hii.
Majina ya kibiashara
Ciclopirox huwa maarufu pia kwa majina ya Loprox na penlac
Fomu ya na uzito wa Ciclopyrox
Ciclopyrox hupatikana kwenye fomu ya mafuta na Shampoo ;
Mafuta huwa na kiini cha dawa kwa aslimia 0.77
Shampoo huwa na asilimia 1 ya kiini cha dawa
Ufanyaji kazi wa Ciclopyrox
Ciclopirox ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) ukuta wan je ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu kwenye ukuta huu na kufanya ukuta uwe dhaifu ambapo hupelekea seli hii kuharibika.
Dawa kundi moja na Ciclopirox
Ciclopirox ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Econazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Miconazole
Naftifine hydrochloride
Oxiconazole nitrate
Sulconazole nitrate
Terbinifine
Terconazole
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazole
Ciclopirox hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi mwilini kutokana na maradhi ya ngozi yanayosababishwa na chawa (Tinea Corporis na pedis )
Hutumika katika maradhi ya ngozi yanayojulikana kama seborrheic dermatitis
Hutumika kutibu candidiasis
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ciclopyrox
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Haipaswi kutumika kwenye macho ,mdomoni na kwenye uke
Upekee wa Ciclopyrox
Ciclopirox hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine.
Nusu maisha ya ciclopirox
Nusu ya maisha Ciclopirox ni saa 1 na nusu baada ya kuingia mwilini.
Ciclopyrox na ujauzito
Ciclopirox hii inaweza kutumika kwa mama mjamzitoendapo faida ni kubwa kuliko madhara ya kitafiti yanayoweza kutokea
Ciclopirox kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa ciclopirox hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya dawa
Baadhi ya maudhi madogo ya ciclopirox pamoja na :
Kuwashwa
Kutokwa na mabakabaka
Kusikia maumivu yanachoma kama moto
Ngozi kuwa kavu
Kutokwa na mapele
Je, kama utasahau dozi yako ya Ciclopirox ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako ya ciclopirox, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda umekaribia wa dozi nyingine, subiria ufike kisha tumia kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-