Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
12 Julai 2020 11:45:51
Dawa ya Flucytosine
Flucytocine ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Ancobon.
Fomu ya dawa Flucytocine
Flucytocine hupatikana kwenye fomu ya kidonge chenye uzito wa miligramu, • 150gm • 200gm
Namna Flucytocine inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa ya Flucytocine hufanya kazi ya kuzuia seli ya fangasi kuingiza ndani vijenzi muhimu vya seli ya fangasi kwa jina la purine na pirimidine. Pia kwa njia nyingine isiyo rasmi huzuia utengenezaji wa DNA na RNA na hivyo seli ya fangasi hufa.
Dawa zilizo kundi moja na Flucytocine
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo; • Amphotericin B • Butoconazole • Capsofungin • Ciclopiro • Econazole • Fluconazole • Griseofulvin • Itraconazole • Ketoconazole • Miconazole • Naftifine hydrochloride • Nystatin • Oxiconazole nitrate • Sulconazole nitrate • Terbinifine • Terconazole • Tioconazole • Tolnaftate • Voriconazole
Kazi za Flucytocine
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.
Dawa zisizopaswa kutumika na Flucytocine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na; • Bacitracin • Deferiprone
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Flucytocine
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao; • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi • Wagonjwa wenye Magonjwa ya figo na mifupa
Utofauti wa Flucytocine na dawa zingine za fangazi
• Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya figo na asilimia kidogo kwenye kinyesi • Dawa hii nusu maisha yake ni masaa 2.4 mpaka masaa 4.8 kwenye mwili.
Matumizi ya Flucytocine kipindi cha ujauzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Flucytocine kipindi cha kunyonyesha
Takwimu Zinaonyesha kuwa haijulikani kwa hii dawa kama inaweza kuingia kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wanaonyonyesha.
Maudhi ya Flucytocine
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Kichefuchefu • Kutapika • Maumivu ya tumbo na kichwa • Kizunguzungu • Kupata Homa • Kuharisha • Kukosa hamu ya kula • kupata maruerue • Kuogopa mwanga • Kuwashwa mwili
Je endapo utasahau dozi yako ya Flucytocine ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-