Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020 12:34:06
Dawa ya Isavuconazole
Isavuconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Triazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Cresemba
Fomu na uzito wa Isavuconazole
Isavuconazole hupatikana katika mfumo wa tembe yenye uzito wa •186mg Isavuconazole hupatikana katika mfumo wa sindano wenye uzito wa
• 372mg/ml
Namna Isavuconazole inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng'enya kinachoitwa saitokromu P-450 ambacho ni muhimu kwa ubadilishaji wa lanosteroli kwenda homoni ergosteroli. Hii inasababisha kupunguza utengenezaji wa ergosteroli, kiungo muhimu katika seli ya fangasi na hivyo kuongeza upenyezaji vitu visivyotakiwa kuingia ndani ya seli ya fangasi na hivyo kufanya zisiendelee kuzaliaana na kufa
Dawa kundi moja na Isavuconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo: • Fluconazole, • Itraconazole, • Posaconazole • Posaconazole • Efinaconazole • Voriconazole
Kazi za Isavuconazole
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.
Dawa zisizopaswa kutumia pamoja na Isavuconazole
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo; • Ecorafenib • Venetoclax
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Isavuconazole
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao: • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi • Wagonjwa wenye Magonjwa ya Ini
Utofauti wa Isavuconazole na dawa zingine kwenye kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (antifangasi aina ya Triazole): • Dawa hii hutolewa mwili kwa njia ya kinyesi kwa asilimia kubwa na kwa njia ya mkojo. • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 130 tangia utumie dawa kunywa kwenye mwili.
Matumizi ya Isavuconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa hali ya hatari ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.Tafiti kwa wanyama zinaonyesha kuwa dawa hii inayo madhara madogo kulinganisha na tafiti za kwa binadamu zinazoonyesha kuwa hakuna madhara yeyote
Matumizi ya Isavuconazole kwa mama anayenyonyesha
Takwimu Zinaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mtoto hivyo inashauriwa isitumike kwa wamama wanaonyonyesha.
Maudhi ya Isavuconazole
Baadhi ya maudhi madogo yanyoweza kujitokeza kwa kutumia dawa hii ni pamoja na : • Kichefuchefu • Kutapika • Maumivu ya tumbo na kichwa • Kizunguzungu • Kuharisha • Kukosa hamu ya kula • Maumivu ya mgongo na kifua • Kuwa na choo kigumu
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-